SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YATOA MKONO WA POLE KWA WALIOKUMBWA NA MAAFA YA MVUA

                                     Na Zahira Bilal Maelezo Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetoa Mkono wa Pole kwa wale wote waliopatwa na ajali na kupoteza jamaa zao kutokana na Maafa makubwa ya mafuriko yaliyosababishwa na Mvua zinazoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine.

Katika taarifa yake iliyotolewa leo na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema Zanzibar imeguswa na msiba huo na kuwaombea majeruhi wa janga hilo wapone haraka na wale waliopoteza ndugu na jamaa kuwa na moyo wa subra katika kipindi hiki kigumu.

Aidha taarifa hiyo inasema kwamba Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Kanda ya Zanzibar Mvua kubwa zitaendelea kunyesha katika maeneo ya Dar es Salaam na maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja na Pemba kwa muda wa siku tatu zijazo.

Kutokana na hali hiyo wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kusafisha mitaro iliyoziba na kuondoka katika maeneo yanayotuama maji ili kuepuka na maafa ambayo yanaweza kujitokeza

Post a Comment

0 Comments