Msanii Dito Bernad na Amini Mwinyimkuu wakicheza pamoja na watoto wanaosoka katika shule ya awali ambayo iko jirani na THT, watoto hao wanasoma katika mazingira magumu wapo wa mtaani , yatima na wanaoishi katika mazingira magumu .Wasanii wachanga na wale wakongwe wa THT waliguswa hivyo waliwatembelea mapema wiki hii na kutoa msaada wa madaftari, kalamu vinywaji baridi kwa watoto sambamba na kucheza nao.Pembeni ya ukuta huo ndipo kuna darasa moja wanalosoma watoto hao ambapo kukuiwa na mvua inabidi kila mtoto abaki nyumbani kwao kwani hakukaliki.Shule hiyo imeanzishwa na msamaria mwema ambaye anahitaji misaada kujengewa majengo na nyenzo zikine mbalimbali zinazohitajika kielimu.
Hapa wakiwa wamewabeba watoto hao ambao waliwalaki kwa kuwarukia na kuwakaribisha kwa kuwaimbia wimbo maalumu.
Watoto wakiwakaribisha wasanii mbele ya darasa lao wa kwanza kulia ni muasisi wa shule hiyo ambaye anasema kila mwezi ada ya mtoto mmoja ni sh.8,000 ambayo inalipwa na wanafunzi wachache tu kutokana na ugumu wa maisha hivyo anahitaji msaada.
Amini akimkabidhi msaada wa viatu mtomto Mummy ambaye alipokea kwa niaba ya wengine .Dito Bernad akikabidhi zawadi ya Juisi kwa mwanafunzi kwa niaba ya wenzake.
Mwakilishi na Ofisa wa Masoko wa THT Daniel Nkya,akiwa ndani ya Darasa la wanafunzi hao ambao wanasoma kwa kupishana muda ndani ya kibanda hiki .Viti wanavyokalia vilitolewa msaada na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.
0 Comments