Mratibu wa Kampuni ya Steps Entertainment Seles Mapunda akiwa na Kanumba.
Mtangazaji wa Kituo Cha Star TV , Sauda , Kanumba na watoto wa Kituo Cha Kulelea Watoto Cha CHAKUWA, klichopo Sinza Mori Dar es Salaam.
Hapa akiwaonyesha watoto mfano wa filamu yake mpya ya The Devil King na kuwaahidi kuwapelekea kopi 100.
Sauda Mwilima na Khadija Kalili hapa tukiwa nje ya nyumba hiyo ya CHAKUWAMA.
Kanumba na mabosi wa Kampuni Steps Entertainment wakiteta jambo.
MSANII galacha wa filamu nchini Steven Kanumba ‘The Great’ jana ametoa sadaka yake kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza Mori Dar es Salaa. Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo Kanumba alisema kuwa ametoa sadaka hiyo kwa watoto hao yatima ambao wanalelewa kituoni hapo siyo kama msanii tu bali anaguswa kwa namna moja ama nyingine. “Mimi natoa sadaka hii ya ftari kwa watoto hao kwa sababu sikumbuki wakati nilipokuwa mdogo kama niliwahi kufurahi hivyo licha ya kuwa mimi nina imani yangu nyingine ya dini lakini ninawajibu wa kutoa hiki nilichojaaliwa” alisema Kanumba. Kanumba aliongozana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Entertainment Jairaj Damodaran na Ofisa Mipango Pritesh Chavda na Mratibu wake Seles Mapunda. Wakati huohuo Kanumba The Great anatarajiwa kuzindua filamu yake ya The Devil King ambayo amemshirikisha msanii anayetamba katika anga la Nollywoo Ramsey Nouah kutoka nchini Nigeria.
Hapa akikabidhi mtoto moja wapo zawadi ambaye aliwawakilisha wenzake.
0 Comments