Social Icons

Thursday, August 4, 2011

ADHA YA KUSHUSHA BEI YA MAFUTA KWA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM HALI BADO TETE

 Kufuatia EWURA kutoa tamko la kushusha bei ya mafuta nchini kote  hali imekuwa ni tete nchi nzima wenye Sheli wagoma kuuza  mafuta na kuleta adha ya hali ya juu kwa wananchi.Hapa ni leo asubuhi Mtaa wa Makunganya na Mkwepu ambako wenye magari wanagombea kununua mafuta ambapo hakuna mwenye hakika kama atapata au la.
 Ni vurugu tupu katika kitika kituo hiki manake kama ni chakula basi watu wanataka kula kwa mikono miwili hakuna utaratibu.
 Kama unavyoona ni ubabe kwa kwenda mbele  katika kununua mafuta hii yote ni kwa sababu wafanya biashara wanatunishiana misuli na serikali  eti kwa sababu tu bei imeshushwa wengine wanadai pump mbovu , na visingizio kibao.
 Ikabidi kila mwenye gari ashuke yaani ni fujoo tuupuu jamani.
 Hakuna maelewano hapa.

Tatizo hili ni la nchi nzima na hadi jana ni Sheli moja tu ya Big Bon ndiyo iliyokuwa ikiuza mafuta bila kutoa visingizio vyovyote. Wafanyabiashara wa Bongo wanashangaza saana siku ikitangazwa mafuta yamepanda bei wanauza bila matatizo lakini sasa imekula kwao imekuwa noongwaa .

No comments:

 
 
Blogger Templates