Huyu ni moja kati ya wasanii chipukizi wa Jiji la Tanga hapa akiwakilisha na kuonyesha vipaji vilivyojificha Jijini Tanga.
Chipukizi wa Jiji la Tanga wakionyesha vipaji kabla ya wasanii waliopagawisha kutoka Dar es Salaam kupanda jukwaani usiku wa leo ambapo tamasha la Serengeti Fiesta linaendelea .
Kimwana Rachel anayetamba na single yake ya Mapenzi Kizunguzungu pia ni zao jipya kutoka Nyumba ya Vipanji Tanzania,Tanzania House of Talent (THT)akionyesha jinsi anavyomudu jukwaa.
Msimu wa dhahabu katika tamasha la Serengeti Fiesta 2011 ukiendelea usiku huu.
Dayna ambaye anatamba na Single ya Mafungu ya Nyanya hapa akiimba na mmoja wa mashabiki wimbo wake wa Mafungu ya Nyanya.
Chiriss wa Malya akipagawisha mamia ya wakazi wa Jiji la Tanga ambao wamejitokeza kwa wingi katika tamasha hilo.
Kundi la Makondoo wakionyesha umahiri wao katika tamasha la leo.
Msanii anayekuja juu hivi sasa kutoka THT, Baker (R.Kelly)wa Bongo kama anavyofahamika kutokana na jumahiri wake wa kumwigiza katika kuimba kadhalika na sauti pia.Wasanii wengine waliofunika ni Bob Junior, Linex na Mama Halima na wengineo wenngi.Wiki ijayo tamasha hili pendwa linalofanyika kwa mara ya kumi sasa limepangwa kufanyika katika viunga vya Leaders Club jijini Dar es Salaam ambako wasanii kochokocho wa hapa nyumbani watatumbuiza bila kumsanii Msanii wa Kimataifa Ludacriss kutoka nchini Marekani atatumbuiza siku hiyo.Wadau tutashangwekajeee hayo ni mambo ya Msimu wa Dhahabu Unaoendelea (Golden Moment).
SERIKALI YASISITIZA UMUHIMU WA MAFUNZO YA UFUATILIAJI NA TATHIMINI KWA
MAENDELEO YA MIRADI YA SERIKALI
-
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) imezitaka
halmashauri, taasisi, na wadau mbalimbali wanaonufaika na mafunzo ya
ufuatili...
4 hours ago
0 Comments