SERENGETI FIESTA MOSHI YAFUNIKA WAKAAZI WAKE WAJITOKEZA KWA WINGI USIKU WA KUAMKIA LEO

Wasanii wanaounda kundi la Kundi la Tip Top Connection wakikamua katika tamasha la Serengeti Fiesta 2011.
Sehemuya umati wa mashabiki ya watu waliojitokeza usiku wa kuamkia leo katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2011 , lililofanyika katika viwanja vya Chuo Cha Ushirika Moshi.

Kundi la Nako2Nako likifanya vitu vyake jukwaani
Picha Zote kwa Hisani ya Ahmad Issa Michuzi wa http://www.jiachie/ .blogspot.com) .

Msanii Godzilla hapa akiimba jukwaani usiku wa kuamkia leo katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2011 lililofanyika kenye viwanja vya Chuo Cha Ushirika Moshi . Mtangazaji wa Clouds Adam Mchomvu a.k.a Baba Johnie akiimba wimbo wake pamoja na mtangazaji mwenzake Reuben Ndege a.k.a Ncha kali.
Msanii Mwendelezo Jaguar kutoka nchini Kenya akiwaimbisha mamia ya mashabiki waiojitokeza kwa wingi katika Tamasha la Serengeti Fiesta wimbo wake rufu wa Kigeugeu unanigeukia Eee katika tamasha la msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta, linaloendelea usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi, na kukonga nyoyo za mashabiki ipasavyo.
Msanii Farid Kubanda Fid Q naye usiku wa kuamkia leo amedhihirisha kuwa mtoto hatumwi ndukani kwa kuchana mistari ipasavyo wakati alipokuwa jukwaani na kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa mkoa wa Moshi.

Post a Comment

0 Comments