Kikosi kazi cha Fiesta katika picha ya pamoja usiku wa leo katika onyesho maalumu la Serengeti Fiesta 2011. Dully Sykes akiimba jukwaani kwa hisia kali usiku huu ndani ya ukumbi wa Royal Village.
Kama kawaida mashabiki wakiguswa na kufurahi huwa hawana hiana hivyo Dully na yeye akapata kilichochake.
Dully Sykes akikamua jukwaani na kibao chake cha Bongofleva kinachotamba hivisasa.
Mkurugenzi Mahusiano wa Kampuni ya Serengeti Teddy Mapunda (Kushoto) na Mkurugenzi Masoko SBL, Caroline Ndungu.
B'12 akiwa jukwaani hapa kitangaza ratiba ya onyesho hilo.
Barnaba na yeye alikuwepo katika kutoa burudani saafi iliyokonga watu na mashabiki waliojitokeza.
Habari Ze'nu bana haina Majotroo, aisee huku dom kweli hakuna Majoto kuna kibariki kikali acha tu, haya wadau hizo ni baadhi ya amshaamsha ya tamasha la Serengeti Fiesta Dodoma ambapo mpangomzima ilikuwa ni katika ukumbi wa Royal Village uliopo Area D, Mkabala na Mlimwa West.
Hapa shabiki na Lina wakienda sambamba .
Lina muimbaji chipukizi lakini ni mkali na mwenye mvuto akiwa jukwaani hapa akiimba na kujiachia kwa raha zake.
Wakienda sambamba hapa ilikuwa ni kibao cha 'Atatamani' .
Mwimbaji nyota lakini chupikizi Esterina 'Lina' akiimba na kucheza na mmoja wa mashabiki waliovutiwa nae.
Mtangazaji wa Kipindi Cha XXL, BTwelve akiwa jukwaani kama Mshereheshaji, kwenye onyesho maalum la Fiesta 2011 ndani ya ukumbi wa Royal Village Dodoma.
Mwimbaji kutoka Mombasa Kenya Nyota Ndogo akitoa burudani katika amsha amsha za Serengeti Fiesta 2011.
Msanii nyota ndogo akiwa jukwaani usiku wa leo, ama hakika alishangiliwa hasa kwa kibao chake cha Watu na Viatu.
Mdau wa Tamasha la Serengeti Fiesta akiwa kajipumzisha akiisikilizia baridi ya mji wa Dodoma.
Mkurugenzi wa Mahusiano Kampuni ya Serengeti Teddy Mapunda akizungumza na waandishi wa habari usiku wa leo kwenye ukumbi wa Royal Village ambapo amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi katika matamasha ya Serengeti Fiesta 2011 yanayoendelea katika baadhi ya mikoa ikiwemo Dodoma ambapo Fiesta itafanyika kwenye uwanja wa Jamhuri.
Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mahojiano mafupi na Mkurugenzi wa Mahusiano Teddy Mapunda. Hapa baadhi ya mashabiki waliofika usiku wa leo kwenye ukumbi wa Royal Village area D Dodoma.
Aisha Shebby, mimi Khadija na Kiongozi kutoka Kampuni ya RnR ,Peter Ngassa.
Mdau kutoka chuo kimoja mkoani hapa Aisha Shebby na mimi tukishow love.
MKUU WA CHUO UDOM AKUTANA NA MENEJIMENTI
-
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Mhe. Stergomena Lawrence Tax (Mb), ambaye
pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, leo ametembelea Chuo
Kikuu ch...
Cara Terbaik Untuk Menang Judi Sicbo Online
-
Bergabung dalam permainan judi sicbo online yang dapat dimainkan melalui
smartphone, maka tentu saja para pemain bisa melakukan sejumlah taruhan
dengan nya...
Waziri Ndalichako azindua chuo kipya cha VETA Kagera
-
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amezindua
chuo kipya cha VETA Ndolage kilichopo Kamachumu Wilaya ya Muleba mkoani
Kagera k...
1 Comments