Mkuu wa Kitengo Cha Mahusiano WCF Laura George.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi katika. Vyombo vya habari Mussa Juma Siwayombe amesema anatoa shukrani za dhati kwaMkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma na wafanyakazi wote wa Mfuko huu kwa kuona umuhimu wa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo haya kwa kundi hili la waandishi wa habari wanachama wa JOWUTA mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
"Binafsi nawashuru wafanyakazi wote wa WCF kwa kufanikisha Mafunzo haya kwani kwa zaidi ya miezi mitatu tulikuwa katika majadiliano ya kufanikisha mafunzo haya na hatimaye leo tarehe 25 Mei 2026 yamefanikiwa na tunaamini hii itakuwa ni mwanzo wa kufanikisha mafunzo kama haya kwa Kanda nyingine, ikiwepo Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Nyanda za juu Kusini.
Mafunzo haya siyo tu yanaimarisha mahusiano yaliyopo kati ya WCF na vyama vya wafanyakazi nchini hasa viilivyopo chini ya mwamvuli wa TUCTA, lakini pia mafunzo haya yanaimarisha mahusiano kati ya WCF na waandishi wa habari na vyombo vyao wanavyofanyia kazi.
Baadhi ya Waandishi wa Habari ambao pia ni wanachama wa JOWUTA wakiwa kwenye mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya Rungwe Sinza Jijini Dar es Salaam.JOWUTA tumaamini mafunzo haya yataongeza uelewa kwa wanahabari na wafanyakazi wote kwa ujumla nchini kupitia habari ambazo zitaandikwa kuhusu masuala mbalimbali ya fidia kwa wafanyakazi .
"Nitumie nafasi hii pia kuupongeza uongozi wa TUCTA Rais wetu, Comrade Tumaini Nyamhokya ,Makamu wa Rais na viongozi wengine, ambao wamekuwa wakitupa ushirikiano mkubwa tangu, tumejiunga na TUCTA mwaka jana" amesema Siwayombe.
"JOWUTA tunaamini ushirikiano wetu, utaendelea ili kuhakikisha tasnia ya habari nchini, wafanyakazi wanapata stahiki zao zote kama ilivyo katika sekta nyingine, lakini pia tunaamini ushirikiano huu, utasaidia sana kutatua changamoto za wanahabari nchini, hasa kutokana na ukweli kuwa zaidi ya asilimia 70 hawana ajira za kudumu wala mikataba ya kazi jambo ambalo ni changamoto kubwa kwa sasa kwa wanahabari nchini".
"Ni vyema mkatambua kwamba WCF ni taasisi yetu sisi wafanyakazi na ipo kwa ajili ya kuhakikisha ustawi wetu hasa pale tutakapopata madhila kutokana na kazi zetu. Mfuko huu wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoanzishwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263]" amesema Mwenyekiti wa JOWUTA.
Lengo la kuanzishwa kwa Mfuko huu ni kushughulikia masuala ya fidia kwa Wafanyakazi waliopo katika sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi wanazozifanya kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao.
"Ninafahamu kwamba WCF inatoa mafao mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za matibabu; fidia ya ulemavu wa muda na ulemavu wa kudumu; malipo kwa anayemhudumia mgonjwa; malipo kwa wategemezi endapo mfanyakazi atafariki; huduma za utengemao; na msaada wa mazishi. Mafao haya yanatolewa kwa wafanyakazi au wategemezi wa wafanyakazi watakaopata ajali, ugonjwa au kifo kutokana na kazi zao. Ndio maana ninawaambia kuwa WCF ni taasisi yetu na hivyo tuna wajibu kuhakikisha tunaulinda kwa nguvu zote kuhakikisha unakuwa himilivu" amesema.
Leo wataalam kutoka WCF watakuwa na siku nzima ya leo kwa lengo kuu moja tu la kuwapatia elimu kuhusu mafao na huduma zote nilizozieleza hapo juu, ikiwa ni pamoja na vigezo na taratibu za madai ya fidia. Hivyo, ninawaomba sana kusikiliza kwa makini wakati wote wa uwasilishwaji wa mada hizi ili mkitoka hapa muende mkawe mabalozi na walimu wazuri kwa jamii kuhusu umuhimu wa huduma zinazotolewa na Mfuko huu.
Amemalizia kwa kuwasihi Wamiliki wa vyombo vya habari nchini, kuwasajili wanahabari katika mfuko wa WCF ili waweze kunufaika na mafao mbali mbali yanayoletewa lakini, pia Niwasihi Wamili wa vyombo vya habari kuzingatia sheria zote za Kazi kwa kuwapa ajira za kudumu wanahabari au ajira za mikataba wanahabari ili nao waweze kunufaika na mifuko ya hifadhi ya jamii na kupata stahiki nyingine.
Lakini pia naomba kurejea kuomba Mfuko wa WCF , kuendelea kutoa mafunzo kwa wanahabari, kwani leo tunawanachama 90 tu wa mikoa miwili Pwani na Dar es Salaam, kati ya wanachama 407 wa JOWUTA nchi nzima, hivyo tuonaomba mafunzo mengine kama haya yatolewe kwa wanahabari katika Kanda nyingine, ambazo ni Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Nyanda za juu kusini, kwani huko pia kuna wanachama na baada ya kupata taarifa za mafunzo haya tumepokea simu nyingi za kuulizwa ni lini mafunzo yatawafikia wao na Waajiri wao, na binafsi kutokana na ushirikiano ambao tunaupata WFC nimewaahidi watafikiwa na kunufaika na mafunzo haya ,Naomba mtufikishie maombi haya ya Mkurugenzi Mkuu.
Kabla ya kumaliza hutuba yangu, pia napenda kuchukuwa fursaa hii, kupongeza jitihada za Serikali katika kutatua changamoto za wanahabari nchini, kwani tumekuwa na vikao kadhaa na Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Waziri wa Kazi na Kamishna wa Kazi na hivi karibuni, msako utaanza katika vyombo vya habari nchini kubaini waajiri ambao, wanawatumia wanahabari bila ajira wala mikataba na tunaamini hatua kadhaa zitachukuliwa na Serikali.
Wanahabari nawakumbusha . Slogan yetu sisi Wafanyakazi Duniani ambayo ni ‘SOLIDARITY FOREVER’ inamaanisha umuhimu wa umoja na mshikamano katika kutetea maslahi ya wafanyakazi. Wafanyakazi ni jeshi kubwa lakini bila kuwa wamoja hatuwezi kufanikiwa katika mapambano ya kudai haki zetu.




0 Comments