Waziri wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga ameagiza Kiwanda cha Viuadudu Cha Tanzania Biotech Production Ltd (TBPL) kinachojihusisha na uzalishaji Mbolea hai kuendelelea kuzingatia ubora katika uzalishaji wa dawa zake.
Kapinga amesema hayo Kibaha Mkoani Pwani katija wa hafla ya utiaji saini za makubaliano baina ya TPBL Kampuni tanzu ya NDC , TFC, TARI, TFRA na TPHPA juu ya ushirikiano wa pamoja.
Aidha Waziri Kapinga ameagiza Menejimenti ya Kiwanda cha Kuzalisha Bidhaa za Kibaolojia Tanzania (TBPL) kinachomilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kupitia Katibu Mkuu kusimamia mpango wa mauzo ya Kiwanda ,"kama alivyoeleza Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo (NDC) Dkt.Nicolous Herman Shombe kuwa uwekezaji wa ni mkubwa lakini uzalishaji ni kidogo ninawataka kuhakikisha tunaongeza ufanisi kwenye masoko ili kuboresha uzalishaji Kiwandani" amesema Kapinga.
Amesema kuwa sifa kubwa mliyosema ya kwamba Kiwanda hiki ni cha kipekee nchini na Barani Afrika hivyo tuzitangaze bidhaa tunazozizalisha kwani uhitaji wa soko ni mkubwa mnahitaji mipango mizuri ya masoko nakuitangaza bidhaa ili iweze kuaminika sokoni na kufungua masoko zaidi na uwekezaji ni biashara.
"Nawaelekeza NDC kuhakikisha tunatumia fursa hiyo kukuza biashara ya kiwanda hiki huku tukihakikisha vipaumbele kwa mataifa ya soko.
Taasisi zilizosaini mkataba wa makubaliano na NDC ni TFC, TARI, TFRA , TPHPA,
na TBPL kuhakikisha yanatekelezwa kwa vitendo na kuleta matokeo yenye manufaa kwa wakulima, sekta ya viwanda na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Waziri Kapinga amesema kuwa mbolea hiyo inasoko kubwa kwani haina kemikali na pia inatunza mazingira hivyo ni salama kwa afya za binadamu pia amesisitiza kuwa izingatiwe ubora wake.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa NDC ambayo ndiyo wasimamizi wa Kiwanda hicho Nicolaus Shombe amesema kuwa uzalishaji wa mbolea hiyo utaleta mapinduzi ya kilimo.
Mkurugenzi Mkuu wa TBPL Mhandisi Rafael Moya amesema kuwa uzalishaji wa mbolea hiyo utasaidia wakulima kuzalisma mazao yasiyo na kemikali kwani kiupaumbele cha Taifa ni kulinda afya za watu.
0 Comments