Kutoka kushoto ni Meneja wa Mambo ya Ndani Kampuni ya Serengeti Imani Lwinga, Mkurugenzi wa Mahusiano SBL, Teddy Mapunda , Mratibu wa Mradi John Mtanda na Meneja Mahusiano ya Jamii Nandi Mwiyombela.
Licha ya kuwa wako Dodoma katika Serengeti Fiesta hawa nia mabosi kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) , kutoka kushoto Nandi Mwiyombela, Mkurugenzi wa Mahusiano Teddy Mapunda na Meneja wa Mambo ya Ndani SBL, Imani Lwinga hapa wakichanganya zege leo kwenye moja ya nyuma za wakoma zilizopo Hombolo Dodoma, SBL wametoa kiasi cha sh. Mil7 ambazo zitamalizia nyumba moja ambayo itachukua familia yenye watu sita.

Kazi ikiendelea ambapo pia SBL, wametoa ahadi ya kujenga kisima cha maji safi na salama kwa wakazi wa Hombolo kitakachogharimu kiasi cha sh. mil30.Mkurugenzi wa Mahusiano SBL, Teddy Mapunda aliyeinama katikati amesema mapema wiki ijayo wataandaa hafla ya uchangiaji itakayofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, kwa lengo la kusaka fedha zaidi huku lengo lao lao likiwa ni kupata sh.mil. 60.
Mratibu wa mradi wa kujenga nyumba za watu wenye ulemavu kutokana na ugonjwa ukoma waishio Hombolo Dodoma , John Mtanda aliyeshika kipaza sauti cha ITV, akizungumza na waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali hawapo pichani , kwamba msaada zaidi unahitajika kwa wakazi hao ambao wamekuwa wakihitaji nyumba za kisasa hivyo watu wenye uwezo wajitokeze. katika kuwasaidia.Mwisho Mtanda aliishukuru Kampuni ya Serengeti kwa kujitolea kujenga kisima na kumalizia nyumba hiyo moja.Kila nyumba inathamani ya sh. mil 13.
0 Comments