KAIMU MNIKULU MKUU MTAWA AKABIDHI BAJAJI 2 ,KWA WASANII WENYE ULEMEAVU WA VIUNGO

Kaimu Mnikulu Mkuu Kassimu Mtawa (katikati) akikabidhi Bajaji mbili zenye thamani ya Sh. milioni 9.5 kwa wasanii wa Kikundi cha Muziki cha Survival Sisters zilizotolewa. Bajaji hizo zilikabidhiwa na Mnikulu Mkuu kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, ikiwa ni utekelezaji wa ombi la wasanii hao waliomtumia. Kushoto ni Irine Malekela na kulia ni Ratifa Abdallah. Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika Ikulu Dar es Salaam leo. Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.
Mmoja wa wasanii wa Kikundi cha Survival sisters, Irine Malekela, akijaribu kuendesha pikipiki ya matairi matatu maarufu kama Bajaji walizokabidhiwa na Kaimu Mnikulu Mkuu Kassim Mtawa, kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, ikiwa ni sehemu ya Rais Kikwete kutekeleza ombi la kikundi hicho la kuwasaidia usafiri utakaowawezesha kuendeleza vipaji vyao vya muziki. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Mnikulu Mkuu Kassimu Mtawa (katikati) akikabidhi Bajaji mbili zenye thamani ya Sh. milioni 9.5 kwa wasanii wa Kikundi cha Muziki cha Survival Sisters zilizotolewa. Bajaji hizo zilikabidhiwa na Mnikulu Mkuu kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, ikiwa ni utekelezaji wa ombi la wasanii hao waliomtumia. Kushoto ni Irine Malekela na kulia ni Ratifa Abdallah. Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika Ikulu Dar es Salaam leo. Picha na Idara ya Habari.MAELEZO.

Post a Comment

0 Comments