WANARUDI NYUMBANI CHIMBUKO LA ASILI YAO

 

Kumekuwa na mwitikio mkubwa wa watalii wa ndani kutembelea hifadhi ya Ngorongoro hii ikimaanisha wanarudi nyumbani eneo ambalo ndilo pekee lenye ushahidi wa kisayansi usiotiliwa shaka kuwa ndio chanzo cha binadamu wa kale.

Safari hii ni zamu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT ) chini ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo Usharika wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam Rev, Dr. Elliona Kimaro aliyeongoza kundi la wanaume 300 kutoka mikoa mbalimbali nchini kutembea Makumbusho ya Jiopaki ya Ngorongoro-Lengai (Urithi Geopark) na vituo vya hifadhi vilivyopo Ngorongoro 

Akiwa na Ujumbe huo Dkt. Kimaro amesema makundi mbalimbali kuhamasika kufanya utalii wa Ndani wanavutiwa na vitu mbalimbali ikiwemo kushuhudia uumbaji wa Mungu, kuona na kujifunza Chanzo cha asili ya Mwanadamu katika bonde la Olduvai na Laetoli, kuona Ikolojia ya hifadhi pamoja na utunzaji wa Mazingira kama vitabu vitakatifu vinavyohimiza.

"Tumekuja Nyumbani Ngorongoro kwenye asili ya Mwanadamu tukiwa na kundi la wanaume 300, tumeshuhudia uumbaji wa Mungu, utunzaji wa Ikolojia, Mazingira, Misitu Wanyama wa kila aina ya vyote vilivyoumbwa kwa mfano wa Mungu" alisema Dkt. Kimaro.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inawarudisha nyumbani binadamu wote ili kushuhudia asili yao ambapo binadamu alianza kutembea na kufanya shughuli zake kwa miguu miwili.

Post a Comment

0 Comments