HIVI KWELI HUU NDIYO USTAARABU WA KUWA MSANII NA KIOO CHA MII????

Msanii wa filamu za Kibongo, Amne Abdul (pichani) ambaye amecheza muvi mbalimbali zikiwemo Simu Sikioni na Kill of Albino, amejidhalilisha na wazazi wake baada ya kuvaa mavazi yaliyoacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake.Amne alinaswa na mapaparazi wetu katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, Dar es Salaam hivi karibuni wakati wa bonanza la wasanii mbalimbali ambapo mwanadada huyo alitinga akiwa amevalia kipensi na kiblauzi kilichoacha sehemu kubwa ya ‘mali’ zake muhimu zikiwa wazi.Awali, msanii huyo alionekana akijivinjari viwanjani hapo akiwa na marafiki zake na katika kujua imekuwaje akavaa vile, mapaparazi wetu walimfuata na kufanya naye ‘intavyu’.Katika majibu yake, mrembo huyo alidai kuwa yeye haoni tatizo kuvaa vile kwa kuwa ameathirika na utamaduni wa kizungu.


(Chanzo http://www.habari/ namatukio.blogspot.com)

Post a Comment

0 Comments