KITUO CHA MAKUMBUSHO SASA CHASUKWA UPYA

Cecy Jeremiah na Khadija Kalili wakiwakilisha katika Kituo hicho ambapo tumebahatika na kuchakuliwa kuwa miongoni mwa wanafamilia wa Kituo hicho na kuwa na jukumu la kuenzi Utamaduni wa nyumbani.

Kutoka kushoto ni msanii nguli pia Mratibu kwa wanahabari Che Mundugwao , katikati ni Mkurugenzi mpya wa Kituo cha Makumbusho kilichopo Kijitonyama Emmanuel Ngallah , anayefuata ni Ofisa Habari Nelly Mbaga na Mtoa Emmanuel wwa Kituo hicho wakizungumza na wanahabari leo katika mlo wa mchana.Ngalla ameeleza wazi mikakati ya Kituo hicho ambapo wamejipanga upya katika kuuenzi na kuutukuza utamaduni wa Mtanzania.Aidha amesisitiza kwa Watanzania kuupenda Utamaduni wao, hivyo kwa kuanzia kila mwisho wa mwei katika kituo hicho kuitakuwa na naa utaratibu wa kuleta vikundi vya ngoma za asili kutoka mikoani katika makabila mbalimbali na wadau wataalikwa wao , watoto ili waweze kuufahamu vyema utamaduni wetu ambao ni urithi kutoka kwa mababu. Ngallah alisema Jumapili washiri wa shindano la Miss Universe wataalikwa katika kituo hicho ambapo watafundwa namna ya kupiga Ngogwe na vyakula vingine vya asili hivyo wapenda misosi siku hiyo jikoni watakuwepo vimwana wakikamilisha mpango mzima wa menu kwa mchana huo.Wakati huohuo anamalizia kwa kusema kuwa kati ya Julai 24 hadi 30 kutakuwa na tamasha la Yakale yanapokutana ya Sasa.




Che Mundugwao hapa akisistiza jambo katika hafla maaklumu ya mlo wa mchana na baadhi ya wanahabari ikiwa ni pamoja na kuunda familia ya wanahabari katika Kituo hicho kwa lengo la kukuza Utamaduni wa Mtanzania.
Mwanaharakati wa Chama Cha Mapinduzi pia Mtangazaji wa Redio Uhuru Cecy Jeremiah na Khadija Kalili hapa tukipata viburudisho vya matunda asilia mchana wa leo na mlo wa Kitanzania ikiwa ni pamoja na Ugali wa unga wa Muhogo wengine huita Bada, Kisamvu Cha Nazi, Walimweupe, Mseto, Ugali wa Mahindi,Walimchanganyiko au waweza sema mseto, Kuku Samaki, mchich, spinachi na kadhalika.



Hapa hii ni meza kaabla ya mlo ambapo imepambwa katika ubunifu wa hali ya juu kwa kutumia mapambo ya Kitanzania kaama unavyoona kuna nyumba za msonge ambazo ni asili ya Mashujaa wa Unyanyembe wenyeji wa Mkoa wa Tabora.




Hapa mimi kulia na Wadau John Badi kutoka gazeti la This Day na Evance Ng'ingo kutoka gazeti la Habari leo tukiwa katika tafakuri ya kuenzi utamaduni wa nyumbani.








Hapa ikiwa tunaapata Chakula Cha Mchana ambapo tulitumia vyombo vya kiasili zaidi vilivyotengezezwa na Mtanzania kama jinsi tulivyovishika.




Mpango mzima wa kukata Bada ukiendelea.








Tukaanza na supu ya kienyeji kwanza ilikuwa nzuri.




Post a Comment

0 Comments