KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YAAPUNGUZA GHARAMA UPIGAJI SIMU ZA KIMATAIFA

Na Mwandishi wetu
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imepunguza viwango vya gharama za mawasiliano kwa wateja wake wanaopiga simu za kimataifa ambapo mteja ataweza kutumia nusu ya gharama baada ya sekunde 120 za kwanza za muda wa maongezi.
Akiongea jijini Dar es Salaam jana Afisa Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando alisema kuwa promosheni hiyo ambayo ni ya siku saba itahusisha nchi za Marekani, Uingereza, Afrika kusini na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
“Ofa hii itausisha nchi nne ambapo kila nchi ina viwango vyake kutokana na kutofautiana katika gharama za kupiga simu katika nchi hizo, lakini lengo letu ni kuhakikisha kuwa wateja wetu wanatumia nusu ya gharama kupiga simu katika nchi hizo tulizotaja baada ya sekunde 120 za awali katika muda wa maongezi” alisema
Mmbando lisema kuwa chini ya ofa hiyo gharama za kupiga simu kwa Afrika kusini itakuwa ni sh 3.76, Falme za nchi za Kiarabu ni sh. 4.32 wakati gharama za kupiga Uingereza na Marekani itakuwa ni Sh. 3.35.
Mmbando alisema kuwa Tigo imeanzisha utaratibu huo wa kupunguza gharama za mawasiliano katika kupiga simu za kimatifa kwa wateja wake na kuogezea kuwa kampuni ya Tigo itakuwa ikifanya hivyo mara kwa mara kwa kuhusisha nchi kadhaa.
Aidha chini ya utaratibu huo Tigo ina mpango wa kutangaza nchi nyingine zitakazofaidika na promosheni hiyo kwa wiki ijayo.

Post a Comment

0 Comments