BAFANABAFANA V TAIFA STARS KUUMANA KATIKA MECHI YA KIRAFIKI MEI 14


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Timu ya Taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ inatarajia kuwasili nchini Mei 12 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania‘Taifa Stars’ itakayofanyika Mei 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar esSalaam.

Nyota wote wa kikosi cha kwanza cha Bafana Bafana kinachofundishwa na PitsoMosimane wanatarajiwa kuwepo kwenye mechi hiyo, isipokuwa kiungo Steven Pienaaranayechezea timu ya Tottenham Hotspurs inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza.

Bafana Bafana na Stars zote zina mechi ngumu ugenini za mchujo kusaka tiketi zafainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) zitakazofanyika mwakani EquatorialGuinea na Gabon. Stars itacheza Juni 4 mwaka huu jijini Bangui dhidi ya Jamhuriya Afrika ya Kati wakati Bafana Bafana itakuwa jijini Cairo, Juni 3 dhidi yawenyeji Misri.

Stars itaingia kambini Mei 7 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo. Wachezaji Idrissa Rajab anayechezea Sofapaka ya Kenya, Henry Joseph (Kongsvinger IL,Norway), Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam),Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada) na Athuman Machupa (Vasalund IF,Sweden) wameshaombewa ruhusa katika klabu zao ili wajiunge na Stars kwa ajili yamechi


MAPATO U23 TANZANIA v UGANDA (THE KOBS)

Pambano la mchujo la All Africa Games kati ya Tanzania U23 na Uganda U23 (TheKobs) lililochezwa Aprili 30 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingizash. 32,982,000 kutokana na watazamaji 24,078 walionunua tiketi.

Watazamaji 22,117walilipa sh. 1,000, 1,749 (sh. 5,000) na 212 (sh. 10,000). Baada ya kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 5,031,152.54 na gharamaza awali za mchezo sh. 16,950,000 mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; uwanja sh.1,100,084.75, gharama za mchezo sh. 1,100,084.75,Shirikisho la Mpira wa MiguuAfrika (CAF) sh. 550,042.37 wakati Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)lilipata mgawo wa sh. 8,250,635.59. Nacho Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata asilimiatano ya mgawo wa TFF ambayo ni sh. 412,531.78.

UCHAGUZI VILLA SQUAD

chaguzi wa klabu ya Villa Squad umepangwa kufanyika kati ya Mei 2 na Juni 20mwaka huu. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imewasilina na Kamati ya Uchaguzi ya VillaSquad na kuitaka kupanga tarehe ya uchaguzi inayokidhi matakwa ya Kanuni zaUchaguzi.

Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi ya Villa atawatangazia wanachama wa Villatarehe ya uchaguzi inayokidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi baada ya kupatamaelekezo ya mchakato wa uchaguzi yaliyotumwa kwake leo.

Tarehe ya Uchaguzi waVilla haitakuwa Mei 22 mwaka huu kama ilivyotangazwa jana na Mwenyekiti waKamati ya Uchaguzi ya Villa Squad. Boniface WamburaOfisa Habari TFF Ref:TFF/ADM/EC.11/---- 03 Mei 2011 MwenyekitiKamati ya UchaguziVilla Squad Football Club.

DAR ES SALAAM YAH: UCHAGUZI WA VIONGOZI WA VILLA SQUAD FOOTBALL CLUB

Rejea barua ya TFF yenye Kumbukumbu Na. TFF/ADM/EC.11/09 ya tarehe 30 Aprili2011 kuhusu somo hilo hapo juu iliyotimwa kwa Katibu wa Villa Squad FootballClub.

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inaaiagizaKamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Villa Squad kuzingatia Kanuni za Uchaguzi zawanachama wa TFF katika mchakato wa uchaguzi uliotajwa hapo juu.

Ili kuhakikisha mchakato huo unafanyika kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi, Kamatiya Uchaguzi ya Villa Squad inakumbushwa kuzingatia viwango vya ada ya fomu zakuomba uongozi na pia tunaambatanisha ratiba ya mfano inayokidhi matakwa yaKanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF kwa urahisi wa rejea na kwa utekelezajiwa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Villa Squad.

Wako katika michezo, Angetile Osiah

KATIBU MKUU

Nakala kwa: KatibuChama cha Mpira wa Miguu

Mkoa wa Dar es salaam

Post a Comment

0 Comments