Social Icons

Wednesday, April 27, 2011

TAMASHA LA PASAKA LAFANA CCM KIRUMBA MWANZA

Christina Shusho akiimba jukwaani jioni ya leo mbele ya wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi kutoka sehemu mbalimbali,ambapo leo ilikuwa ni siku ya Muungano,lakini limefanyika tamasha la muziki wa injili,lililoandaliwa na kampuni ya Msama Promotions kwa ajili ya wakazi wa jiji la Mwanza ambapo wakazi wake bado walikuwa mapumzikoni


Anaitwa Bonny Mwaitege ambaye kwa sasa anatamba na nyimbo zake kadhaa ikiwemo ule wa Mama ni Mama pamoja na Njoo ufanyiwe maombi,nyimbo ambazo pia jioni ya leo ameziimba mbele ya wakazi wa jiji la Mwanza. Wakazi wa jiji la Mwanza wakishangilia kwa nguvu huku baadhi yao mikono yao ikipunga hewani,jioni ya leo kwenye tamasha la muziki wa nyimbo za injili lililoandaliwa na kampuni ya Msama Promotions,ya jijini Dar Es Salaam. Mwimbaji nyota wa muziki wa nyimbo za injili,Anastazia Mukabwa ambae kwa sasa anatamba na wimbo wake wa kiatu kivue alioshirikiana na Rose Muhando,akiimba jukwaani jioni ya leo kwenye uwanja wa ccm-kirumba,ambapo ilikuwa ni muendelezo wa tamasha la pasaka lililoanzia jijin Dar,kisha Dodoma na kumalizikia jijini Mwanza,ambapo ilikuwa ni siku ya sherehe za muungano kati ya Tanganika na Zanzibar. Baadhi ya nyota wa muziki wa injili,kutoka kushoto ni Rose Muhando,Christina Shusho pamoja na Solomon Mukubwa wakijadiliana jambo kabla ya kupanda jukwaani jioni ya leo kwenye uwanja wa ccm-kirumba,jijini Mwanza. Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama (waandaaji wa tamasha) akimsikiliza kwa makini mmoja wa watangazaji mahiri wa Clouds FM (kituo cha Mwanza),Albert Sengo kuhusiana na albamu mpya ya Anastazia Mukabwa aliomshirikisha Rose Muhando,iitwayo Kivue kiatu,pichani kati ni mfanyakazi wa Clouds FM ndani ya jiji la Mwanza aitwaye Samadu akisikiliza pia.




Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka DRC-Kongo Faraja Ntaboba akizikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa nyimbo za injili jioni ya leo,kwenye tamasha hilo lililofanyika katika uwanja wa ccm kirumba,jijini Mwanza na kuhudhuriwa na watu kibao.


Nyota mwingine wa nyimbo za injili kutoka nchini DRC-Congo,Solomoni Mukubwa akiwaimbia wakazi wa jiji la Mwanza jioni ya leo kwenye tamasha la nyimbo za muziki wa injili lililowakutanisha wakazi mbalimbali jioni ya leo,ambapo ilikuwa ilikuwa ni siku ya Muungano.

1 comment:

Anonymous said...

Je gwiji wetu tunayejivunia ktk muziki wa injili hapa bongo yu wapi??? Tunaona wasanii wengi hata wa nchi jirani WAKITAMBA, lakini hatumuoni Cosmas Chidumule !!! kulikoni??au ndio amefulia kimuziki??? Inashangaza kuwa gwiji huyu alipokuwa akiimba muziki wa dansi alikuwa akisikika sana cha ajabu ameingia ktk muziki wa injili hasikiki tena !! au labda kutokana na imani za kuokoka kwake kuwa kushiriki ktk tamasha la aina hii ni DHAMBI ??

 
 
Blogger Templates