TAMASHA LA FIESTA SOKA BONANZA LAFANA LEADERS CLUB ,KARUME DAY

Ofisa Masoko wa Bia ya Tusker inayotolewa na Kampuni ya Serengeti (SBL) ,Caroline Ndungu hapa akitoa maelezo mafupi kuhusu tamasha hilo ambalo ni mwanzo na utambulisho wa matukio kibao katika safari ya kuelekea tamasha la Fiesta 2011. Mratibu wa Tamasha hilo la Fiesta Soka Bonanza Shafii Dauda kutoka Clouds Media Group.
Mwenyekiti wa Arsenal Tanzania Said Tulliy kushoto, mimi Khadija na Luambano wa Clouds FM Redio.


Hapa ilikuwa ni timu ya Chelsea Tanzania wakishjangweka kimpango wao.
Camera yangu iliguswaa upande huuu na ushindani ulikuwa siyo wa kutania kwani kila timu ilikuwa imepania kushinda.
Hapa tukishow Love na watoto ambao nao hakuwtaka kubaki nyuma kutoka kushoto ni B 12, Jimmy wote watangazaji wa Redio Clouds Mimi, Vanessa na Wilfred Mwakalebela pamoja na Ndimbo Junio na huyo baby mdogo kuliko wote nilishindwa kupata jina lake kwani alikimbia mara baada ya kuona wenye kamera zao wamemaliza zoezi.

Baadhi ya Wachezaji wa timu ya Arsenal Tanzania wakifurahia kupigwa picha.
Blogger pia muasisi wa Blog nchini Ankal Muhidin Issa Michuzi wa Michuzi Blogspothapa akiwa kajichanganya na mashabiki wa Bwawa la Maini.

Ankal kazini na ushabiki kama kawaa.
Baadhi ya Vijana wa Barcelon ambao walionyesha kabumbu la kufa mtu leo Leaders Club.
Hapa kutoka kushoto ni Mtangazaji wa Kipindi Cha XXL B Dosen Redio Clouds FM, mimi Khadija, Wilfred Mwakalebela na Jimmy mtangazaji wa redio Clouds FM.
Mashabiki na wachezaji wa timu ya Chelsea Tanzania.

Inter Milan nao hawakubaki nyuma katika bonanza hilo liliovutia wengi Jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Real Madrid hapa ni mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Leaders Club tayari kwa mechi.

Watani Machester United hapa wakavamia banda la timu ya Arsenal na kuanza kucharuana.
Hiki ndichi Kikosi cha timu ya Arsenal Tanzania kilichishuka dimbani leo ilikuwa ni raha kila wakati ambapo timu hiyo iliposhuka dimbani.
Wachezaji na mashabiki wa timu ya AC Milan hapa mara baada ya kuingia katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni.
Rapa wa bendi ya Mashujaa Ibrahim Mindinda Nyeusi akichacharika jukwaani licha ya kuwa na mvua lakini mambo yalikuwa shega tu.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Frederick Mwakalebela ambaye ni mmoja wa washauri wa timu hiyo ya Chelsea Tanzania hapa wakijadili jambo.
Sehemu ya maandamano leo asubuhiambayo yalianza katika viwanja vya Biafra hadi Leaders Club.
Police Brass Band ndiyo walioongoza msafara huo huku nyuma zikifuata timu nane zenye mashabiki Ulaya.
Paul James Mtangazaji wa Redio Clouds hapa akiwa kazini ambapo kituo hicho cha redio kilikuwa kikirusha matangazo yake moja kwa moja kila lililojiri katika viwanja vya Leaders.

Ahmad Issa Michuzi 'Michuzi Junior' wa Blog ya Jiachie yeye aliamua kupanda juu ya gari hili la kurushia matangazo ili apate picha nzuri zaidi.

Post a Comment

0 Comments