Kiongozi wa bendi ya Jahazi Modern Taarab Mzee Yusuf , ametangaza kusitisha maonesho ya bendi hiyo kwa siku chache ikiwa ni katika kuomboleza msiba wa wasanii 13 waliofariki kwenye ajali iliyotokea Morogoro jana usiku.Mzee Yusuf amesema ameguswa sana na msiba huo mkubwa hasa ikizingatiwa kwamba karibu wasanii wote waliofariki alifanya nao kazi huku wengine wakiwa ni wanafunzi wake kama marehemu Issa Kijoti ambaye alijipatia jina na umaarufu wakati alipokuwa na Jahazi kabla hajahama na kwenda Five Star hadi mauti yalipomfika.Aidha Mzee alisema kwamba yuko radhi hata kurudisha fedha alizopokea kama malipo kwa Jahazi kufanya maonesho.
0 Comments