Habari za usiku huu wadau ,habari zilizopatikana hivi sasa ni kwama kuna mama mjamzito umri haujatajwa mkazi wa Bunju B Jijini Dar es Salaam.Jina na umri havikupatikana amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye choo alipokwenda kujisaidia leo.Kwamujibu wa taarifa iliyopatikana huku chanzo kikiwa ni Kituo cha ITV,mama huyo alisikika akipiga kelele za kuomba msaada na mara bada ya majirani kufika eneo la tukio, walikuta ukuta wa choo ukiwa umebomoka na mama katumbukia walitoa taarifa Polisi ambapo walipofika katika eneo la nyumba hiyo waliishia kuopoa mwili wa mjamzito huyo ambaye tayari alikwisha poteza masiha.Kutokana na tukio hilo wenye nyumba wameshauriwa kujenga vyoo imara ikiwa ni pamoja na kufanya ukarabati wa majengo na ukaguzi wa mara kwa mara ili kunusuru maisha ya wapangaji.
CHEZA 100 SUPER ICY USHINDE KITITA KIZITO
-
LEO ndio ile siku ambayo unaweza kushinda kitita cha kutosha kwani
wataalamu wa michezo ya kubashiri kampuni ya Meridianbet kupitia Sloti ya
100 Super Ic...
12 minutes ago
0 Comments