MAMA YANGU UTABAKI KUWA NGUZO YA MAISHA YANGU MPAKA SIKU YANGU YA MWISHO KATIKA MAISHA YANGU HAPA DUNIANI NAJUA KWAMBA WEWE NDIYE ULIYEKUWA UKITOA TABASAMU LA KWELI KATIKA MACHO NA UVUNGU WA MOYO WAKO KWANGU.NI VIGUMU KUKUSAHAU LAKINI SINABUDI KUSEMA KWANI NAJUA KILA NAFSI LAZIMA ITAONJA UMAUTI NA DAIMA NA MILELE UTABAKI KUWA MALIKIA KATIKA MTIMA WANGU.JAMANI MAMA ANAUMA, MAMA ANARAHA YAKE ACHENI MAMA AITWE MAMA NA HAKUNA KAMA MAMA. WAKATI MWINGINE HUJIKUTA NASHIKWA NA DONGE LA UCHUNGU ROHONI NA KUBUBUJIKWA NA MACHOZI HATA KAMA NIKO WAPI HASA NINAPOMKUMBUKA KUTOKA NA KUKOSA UCHESHI WAKE,UKALI WAKE PIA ALIKUWA NI MTU ALIYEWEZA KUTOA MANENO YA KUFARIJI HASA PALE UNAPOKWAMA AU KUPATA MISUKOSUKO YA MAISHA NA KIDUNIA NILIKUKIMBILIA MAMA AMBAPO ALINIPA NGUVU ZA MANENO NA KUNITOLEA MIFANO YA MAPITO MENGI KATIKA MAISHA LAKINI SASA NIMEBAKI AU NISEME TUMEBAKI WAKIWA NA TUKIBAKI KUMSHUKURU MUNGU KWA YOTE.ILIKUWA SIKU KAMA YA LEO MIAKA MIWILI NYUMA HAKIKA HAKUNA ATAKAYEISAHAU KATIKA FAMILIA YETU WATOTOT NA WAJUKUU WAKE .MARA BAADA YA KUFARIKI ALFAJIRI YA SIKU KAMA YA LEO ALIZIKWA ALASIRI SIKU HIYOHIYO KATIKA MAKABURI YALIYOPO KIBAHA,MKOANI PWANI . KWA NIABA YA WENZANGU TUNAWASHUKURU WOTE WALIOKUWA PAMOJA NASISI KWA KUTUFARIJI KWA NJIA MOJA AU NYINGINE KATIKA SIKU ILE ILIYOJAA TAHARUKI,INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAJIUN.
UFANYAJI WA MITIHANI YA 29 YA PSPTB WAKAMILIKA
-
Bodi ya wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imeendesha mitihani yake ya 29
kwa jumla ya watahiniwa 1,223 katika ngazi za Professonal Diploma, Graduate
...
1 hour ago
2 Comments