ASALAAM Aleykum mpenzi msomaji wangu wa safu hii adimu na adhimu ya Busati la Wikiendi ikujiayo mara moja tu kwa wiki katika siku kama ya leo?
Sina shaka sote, ninyi pamoja na mimi ni wazima wa afya, ambako kwa wale wenzetu ambao kwa namna moja ama nyingine hawakujaaliwa kuamka salama, nachukua fursa hii kuwapa pole.
Tabia ya baadhi ya bendi na makundi mbalimbali ya muziki hapa nchini kuwanyanyapaa waandishi wa habari, inaonekana kuzidi kukomaa na kuota mizizi kwa kiasi kikubwa kadri siku zinavyozidi kusonga.
Licha ya kuwa, hili lilishapigiwa kelele mno na mara nyingi kwelikweli na waandishi wenyewe wengi kupitia kalamu pamoja na vipaza sauti vyao.
Mara nyingi bendi, vikundi vya muziki na hata wasanii wenyewe huwa wakarimu na wenye kauli nzuri za kubembeleza pale tu wanapokuwa wanahitaji msaada wa kutangaziwa maonyesho yao tu.Lakini, malengo yao yanapotimia hugeuka na kuwa si waungwana hata kidogo ambako husahau kuwa, mchango wa wanahabari ni sehemu kubwa ya mafanikio ya tukio lao zima.Aidha, wakati mwingine wamiliki wa makundi hayo ya muziki wanapoulizwa hujibu kuwa, ni kwasababu baadhi ya maonyesho hukodiwa na hivyo hukabidhi majukumu yote ya siku hiyo kwa wateja wao.
Nimeamua kulisema hili leo kutokana na kupokea malalamiko mengi kutoka kwa waandishi pamoja na watangazaji wengi wanaodai kunyanyaswa na makundi ya muziki.
Katika hilo bado kuna nafasi kubwa ya wamiliki hao kutupiwa zigo zito la lawama, kwasababu kwani hao wanaowakodisha bendi zao kwa ajili ya matamasha yao huwa hawawapi kanuni nma misingi ya kazi zao.Kwamba, kuna vyombo vya usalama kama vile polisi, viongozi wa vyama mbalimbali vya sanaa pamoja na sisi wanahabari ambao kwa namna moja ama nyingine ni muhimu kwao kwa siku zote?Bila kuficha, hii ni dharau tu ya baadhi ya wasanii wetu wanaoona kuwa umuhimu wa wanahabari huishia siku moja kabla ya matamasha yao.Kwasababu, wakati mwingine wanahabari hudhalilishwa na mabaunsa huku wenyewe wamiliki wakishuhudia bila kuonyesha jitihada za kuwasaidia kwa namna moja ama nyingine.Sana sana inapotokea wamiliki hao kushuhudia tukio la mwanahabari kudhalilishwa na mabaunsa, hugeuka na kuwa upande wa hao wanaowaita wateja wao, yaani mapromota wa onyesho.Hudiriki kusema kuwa, wanahabari hao ndio wakorofi na kwamba wanavigeuza vyombo vyao kama bakora ya kuwaadhibu wasanii kila pale wanapojisikia kufanya hivyo.Ikumbukwe kuwa, mwanahabari hana mipaka katika kazi yake, ambako kitendo cha yeye kuzuiliwa kuingia mahala kufanya kazi yake kwa ujumla ni kumnyima uhuru.Kadhalika, ni kuikosesha jamii taarifa muhimu ambazo zingepatikana katika tukio hilo lililokuwa likiwaniwa na mwanahabari husikakulishuhudia kwa wakati muafaka.Inashangaza mno kwasababu, mnapokuja kuomba kutangaziwa matamasha yenuhutushawishi tuje kwa wingi katika matamasha hayo huku mkidai ya kuwa hakutakuwa na vikwazo.Laiti kama si bilisi wangu kukaa mbali kidogo kwa leo, ningewaanika hadharani wale wasanii na makundi yote ambayo ni vinara wa tabia hiichafu, lakini yote kwa yote nawataka mjirekebishe.Kwakuwa, sote tunafanya kazi kwa kutegemeana, yaani nyinyi mnatutegemea sisi katika kuwatangaza, na sisi pia tunawategemea ninyi ili kupamba vyombo vyetu vya habari.Lakini mtambue kuwa, nyie ndio mko wengi zaidi, ambako tunaweza kuwaacha nyie mnaoonekana kuwa si waungwana kwetu tukafungamana tu na wale tunaofanana nao kitabia.Na hata kama tutaamua kuachana na ninyi nyote bado itakuwa hakuna madhara kwetu kwasababu tunaweza tukavigeuza vyombo vyetu kuwa ni vya kutangaza na kuandika soka pamoja na michezo mingine peke yake.
WAZIRI AWESO AIAGIZA DAWASA KUHAKIKISHA WANANCHI WA MANGA HANDENI
KUUNGANISHWA MAJI
-
Na Oscar Assenga,Handeni.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameiagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Dar es Salaam ( Dawasa) kuhakikisha wananchi wa e...
3 hours ago
0 Comments