Social Icons

Friday, February 11, 2011

BENDI YA KALUNDE SHEREHEKIA MIAKA 5, VALENTINE'S DAY

Kiongozi wa Bendi ya Kalunde Junior Gringo kushoto akiwa na Rai wa Bendi hiyo Deo Mwanambilimbi nje ya Ukumbi wa MAELEZO.
*****************************************************************************
RAIS wa bendi ya muziki wa dansi Kalunde Deo Mwanambilimbi amewataka mashabiki na wadau wa muziki kujitokeza katika onyesho lake la siku ya Wapendanao Valentines Day itakatokwenda sambamba na kusherehekea miaka mitano ya bendi hiyo.Mwanambilimbi almaarufu kwa jina la Mzee wa Goba ameyasema hayo leo asubuhi nje ya ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO Jijini Dar es Salaam, kuwa mambo yakuwa bambam siku hiyo.Katika sikukuu ya Valentine Kalunde imepanga kusherehekea siku hiyo kwa mtindo wa kipekee kwenye ukumbi wa Rain Bow Kawe Jijini. Aliongeza kwa kusema kuwa mashabiki wajitokeze kucheza ngoma zao kali kama Itumba Nwewe, Nataka Kuzaa na Wewe, `, Fikiria, Naomba Uniambie, Umenigusa na nyinginezo bola kusahau kusakata mtindo wa Lekelembuke. Naye Kiongozi wa bendi hiyo, Junior Gringo alisemaonyesho hilo ni maalum kwa mashabiki wao pamoja na bendi. Aidha zawadi mbalimbali zitatolewa kwa mashabiki watakaofika, ambapo wasanii wa filamu nchini Ray Kigosi 'Ray' na Steven Kanumba 'The Great’ watatoa zawadi kwa mashabiki. Mbali ya wasanii pia watu mashuhuri kutoka katika kila nyanja watakuwepo. Wakati huohuo Kalunde wanatarajiwa kutambulisha nyimbo zake nne mpya ambazo zimekamilika. Alizitaja nyimbo zitakazotambulishwa siku hiyo kuwa ni ‘Nyemo’ ambayo imeimbwa kwa lugha ya kabila la Kigogo wenyeji wa mkoa wa Dodoma na uliotunga wa Sarafina Mshindo.
Nyimbo nyingine ni ‘Gloria’ iliyotungwa na Shehe Mwakichui, ‘Ndoto’ imeitungwa na Gringo na ‘Masumbuko’ utunzi wake Deo Mwanambilimbi.Gringo anaongeza kwa kusema kabla ya kufika siku hiyo ya Valentine, kesho itawatambulisha wanamuzi wake wapya pamoja na wanenguaji wake waliokuwa Muscat Oman katika onyesho huohuo wa Rainbow. Aliwataja wanamuziki watakaotambulishwa kuwa ni Remmy Gius ambaye ni mwimbaji na mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Edson anayekung'ukuta gita la solo.

No comments:

 
 
Blogger Templates