Wakati fainali za taifa za shindano la Miss Utalii Tanzania zimepangwa kufanyika usiku wa Februari 5, 2011, mrembo atakayenyakua taji la taifa la Miss Utalii mwaka huu ataondoka na faida kubwa ya zawadi ya mkataba wenye thamani ya shilingi milioni mia moja na hamsini.
Taarifa iliyotolewa na Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo imeeleza kuwa, shindano la mwaka huu litafanyika kwenye hoteli ya kitalii ya Kiromo View Resort iliyopo umbali wa kilometa kumi tu toka Bagamoyo mjini ambapo pia kutakuwa na burudani kadhaa zitakazosindikiza usiku huo adhimu na ya kihistoria katika tasnia nzima ya urembo na utalii hapa Tanzania.
Akaendelea kusema; washiriki wote wa fainali za Miss Utalii Tanzania 2010/11 wako katika hali nzuri kiafya na kisaikolojia kwa ajili ya shindano na kufafanua kuwa mbali ya kitita hicho kwa Malkia wa mwaka huu, warembo wengine wataweza kujitwalia mataji yatakayowakilisha hifadhi za taifa 16 zilizo chini ya mamlaka ya hifadhi za Taifa (TANAPA).
Taarifa iliyotolewa na Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo imeeleza kuwa, shindano la mwaka huu litafanyika kwenye hoteli ya kitalii ya Kiromo View Resort iliyopo umbali wa kilometa kumi tu toka Bagamoyo mjini ambapo pia kutakuwa na burudani kadhaa zitakazosindikiza usiku huo adhimu na ya kihistoria katika tasnia nzima ya urembo na utalii hapa Tanzania.
Akaendelea kusema; washiriki wote wa fainali za Miss Utalii Tanzania 2010/11 wako katika hali nzuri kiafya na kisaikolojia kwa ajili ya shindano na kufafanua kuwa mbali ya kitita hicho kwa Malkia wa mwaka huu, warembo wengine wataweza kujitwalia mataji yatakayowakilisha hifadhi za taifa 16 zilizo chini ya mamlaka ya hifadhi za Taifa (TANAPA).
Kadhalika, Chipungahelo amesema kuwa mbali ya mataji ya hifadhi, pia, kutakuwa na tuzo zingine toka baadhi ya makampuni na taasisi zilizodhamini shindano hili ili kuyawakilisha katika suala zima la kuutangaza utalii kupitia hifadhi za taifa na utamaduni wa Mtanzania na hivyo kuongeza hamasa zaidi kwa washiriki ambao nao wameonesha kujawa shauku ya kufanya vema.
“Fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2010/11, zitakuwa tukio kubwa zaidi la kitaifa la kitamaduni na urembo nchini, ambalo kishindo chake kitaleta mageuzi makubwa katika sanaa ya urembo nchini, barani Afrika na duniani kwa ujumla. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa mara ya kwanza dunia itashuhudia idadi kubwa ya warembo wakiwa jukwaa moja wakitangaza na kuonesha utamaduni kupitia mavazi ya asili, ya kitalii, ya mitindo, ya ubunifu. Pia, warembo hao wataonesha vipaji vya kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za asili za mikoa au kanda wanazowakilisha,’ amesema Rais wa Miss Utalii Tanzania.
Aidha, amewataja wadhamini wakuu wa shindano la taifa la Miss Utalii 2010/11 ni Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,Business Times Limited, Kiromo View Resort na Sahara Media Group Limited,inayomiliki kituo cha runinga cha Star TV, Radio Free Africa, Kiss FM na gazeti la Msanii Afrika. Wengine ni Zizzou Fashion, Alaisy Travel, Auckland Tours, Tintona TankStation, Tesco Furniture, Mlonge By Makai Enterprises,Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Coco Beach.
Warembo hao wameanza ziara rasmi za kutembelea na kutangaza vivutio vya utalii ,kwa kutembelea maeneo ya kihistoria yaliyopo Mkoani Pwani,ambapo juzi walitembelea Maeneo ya Kihistoria yaliyopo wilayani Bagamoyo ikiwemo Magofu ya Kaole,wakiongozwa na katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo. Aidha jana warembo wote 60 walitembelea na kutangaza Fukwe za Bahari ya Hindi zilizoko mkoani Dar Es Salaam wakiongozwa na Mbunge wa Kinondoni Mh, Idd Azan. wakiwa katika Fukwe wa Coco Beach warembo hao wakiwa wamegawanywa katika timu nne za mpira wa miguu walishindana kusakata kabumbu la Ufukweni hali iliyopelekea kuwa kivutio kikubwa na kusababisha ufukwe huo kufurika mamia ya watu wakishuhudia warembo hao wakionyesha vipaji vya hali ya juu ya kusakata kandanda.
michuano baina ya timu hizo za warembo zilizopewa majina ya hifadhi za Taifa ulikuwa mkubwa na kuamsha shangwe za mara kwa mara kwa wapenzi waliojazana kushuhudia mechi hizo. katika mchezo wa kwanza timu ya soka ya warembo wa Ngorongoro iliweza kuibwaga timu ya soka ya Selous kwa mabao 4-2 wakati katika mchezo wa pili ambao ulizikutanisha timu za Serengeti National Park dhidi ya Maunt Kilimanjaro na matokeo timu ya Mlima Kilimanjaro kuibuka kwa ushindi wa mabao 3-1. Mbunge wa Kinondoni Mh, Idd Azan kwa kufurahishwa na viwango vilivyoonyeshwa na timu hizo za warembo wa miss Utalii Tanzania 2010- 2011 ambao tarehe 5 mwezi wa pili watapanda jukwaani kuwania taji la Miss Utalii Tanzania 2010- 2011 katika Hotel ya Kitalii ya Kiromo Bagamoyo, alinunua kila goli kwa shilingi elfu kumi(10,000) hivyo aliweza kutoa shilingi laki moja kwa magoli kumi yaliyofungwa. naye mfanyabiashara maarufu nchini Zizzou Fashion alitoa seti nne za jezi kwa warembo wote 60.
0 Comments