Mkurugenzi wa THT Ruge Mutahaba akimkaribisha ukumbini aliyekuwa Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Michezo Utamaduni na Vijana Dk. Emmanuel Nchimbi, katikati ni Mkurugenzi wa Utamaduni wa Wizara hiyo Profesa Hermans Mwansoko.
Wasanii sita waliozindua rasmi albamu zao usiku wa kuamkia leo katika hafla mwanana iliyofanyuka kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam kutoka kushoto ni Amini, Mwasiti,Dito,Matalima,Barnaba na Lina.Uzinduzi huo ulihudhuriwa na watu mashuhuri akiwamo Waziri Mkuu Msataafu Edward Lowassa na aliyekuwa mgeni Rasmi Waziri wa Habari Utamaduni na Dk. Emmanuel Nchimbi. (Picha zote na blog ya http://www.fullshangwe/.blogspot.comna www.JaneJohn5.blogspot.com)
****************
Uzinduzi wa albamu sita kali za wasanii wa Nyumba ya Kuvumbua Vipaji vya Wasanii wachanga Tanzania ‘Tanzania House Of Talent’ (THT), uliofanyika katika mkesha wa sikukuu ya miaka 47 ambayo ni kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar umetia fora kutokana na namna ulivyokuwa.
Tanzania Daima ambayo ilikuwepo katika ukumbi huo na kushuhudia wasanii wake wakitia fora ambao ni Mwasiti, Mataluma, Barnaba, Amini, Linah na Dito wote kwa umoja wao wameonyesha jinsi walivyo mahiri na kuiva kisanii baada ya kupikwa na waalimu wa THT.
Wasanii walioweza kuamsha hisia katika nyimbo zao ni pamoja na Mataluma aliyebamba na ngoma yake ya Kariakoo, huku mwasiti ikivuta hisia za mashabiki kwa wimbo wa Nalivua pendo na Siyo kisa Pombe.
Ukiacha Mwasiti naye Dito alikuja na kuwashika mashabiki kwa wimbo wa huku Barbnaba akizidi kuonogesha tukio hilo kama hiyo haitoshi naye mwana dada Lina alikuja na kukimbiza na ngoma yake ya Bora nikimbie wimbo ambao unazungumzia kadhia za mapenzi ambapo katika wimbo unawakilisha kilio cha mwanamke ambaye baada ya kuoma mambo yanakuwa magumu kwa mpenziwe kutokana na vipigo , ulevi na karaha mbalimbali kutoka kwa mpenzi wake anaona bora akimbie huku akisema ‘Kama Mapenzi ndiyo haya naona bora nikimbie nimechoshwa na vituko na vipigo majeraha kila siku mpenzi wangu kwa ninii hunithamini”.Wimbo huo wa Lina ulikuwa ni miongoni mwa nyimbo zilizogusa wengi, hakika kila msanii aliyepanda jukwaani alibamiza kivyake na kuacha historia kwa tuliokuwa mashuhuda pale Mlimani City.
Aidha Mratibu wa tamasha hilo la kihistoria, Kemmy Mutahaba ambaye pia ni Msemaji wa THT, amewatoa shukrani za dhati kwa vyombo vya habari , mashabiki na watu wote waliojitokeza kwa wingi katika kuona kazi za nyumba hiyo iliyoanzishwa miaka mitano uliyopita.
Wasanii wengine walionogesha kwa kutoa burudani ni pamoja na bendi ya Odama, Banana Zorro, Marlow, Maunda Zorro, Pipi ,Beka na Wanenguaji wa THT.

Mtangazaji wa kipindi cha Power Break Fst Babra Hassan akiwa na wadau katika uzinduzi huo ambapo wadau wamehimizwa kununua kopi Original ili kuwapa sapoti wasanii wetu na siyo kununua albamu za kughushi.
Aliyekuwa Mtangazaji mahiri wa kituo cha Redio Clouds Gadna G. Habash akipata kiburudisho kabla ya kuanza kwa onyesho.Ilikuwa hivi ukiingia tu katikla lango mara baada ya kukaguliwa kadi yako kila mmoja alikaribishwa kuchagua aina ya kinywaji unachotumia yaani aina yoyote watu walipatiwa baada ua hapo tukaingia nadani nako baada ya muda makulaji yakaletwa mezanii tukajisevia taratiibu huku tukifurahia shoo.
0 Comments