Kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta Luiza Mbutu akiwa na Msanii Juma Kassim 'Sir Nature' mara baada ya mkutano wa waandishi wa habari na waandaji wa Tamasha la Sauti Za Busara JTwanga na Sir Nature wote watakuwepo katika tamasha hilo la Sauti za Busara kwa mara ya pili wakati Twanga watakuwa Zenji kwa mara ya kwanza.
Sauti za Busara ni moja ya matamasha yenye mvuto wa kipekee barani Afrika, mwaka huu litafanyika kwa mara ya nane visiwani Zanzibar katika Mji Mkongwe kuanzia Februari 9-13.Tamasha hili hukutanisha watu wa tamaduni mbalimbali na kuwaweka pamoja, wakisheherekea na kufahamiana kama alivyosema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya ufunguzi wa tamasha la mwaka 2010.“tukio hili ni muhimu kwa kuwa linatoa fursa kwa wageni na wenyeji wa tamaduni mbalimbali kubadilishana mawazo,kuonyeshana upekee wao, utajiri na utofauti wa muziki wetu. Kwa ujumla linachangia kuimarisha muingiliano wa tamaduni na urafiki.”Sauti za Busara huwakutanisha wasanii wakubwa wa muziki barani Afrika pamoja na kuibua vipaji vingine nchini. Mwaka huu vikundi 40 vitatumbuiza, baadhi ni, Orchestre Poly Rythmo de Cotonou (Benin), Blick Bassy (Cameroon), Otentikk Street Brothers (Mauritius), African Stars Band aka Twanga Pepeta (Tanzania), Mlimani Park Orchestra (Tanzania), Kwani Experience (South Africa), Culture Musical Club (Zanzibar), Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta ft. Bi Kidude (Zanzibar), Jagwa Music (Tanzania), Bismillahi Gargar (Kenya), Maulidi ya Homu ya Mtendeni (Zanzibar), Djeli Moussa Diawara (Guinea), Christine Salem (Reunion), Yaaba Funk (UK), Muthoni The Drummer Queen (Kenya), Jahazi Modern Taarab (Tanzania), Les Frères Sissoko (Senegal), Sukiafrica Sukiyaki Allstars (Pan Africa / Far East), Groove Lélé (Reunion), Vusa Mkhaya & Band (Zimbabwe / Various), Djaaka (Mozambique), Nomakanjani Arts (Zambia), Percussion Discussion Afrika (Uganda), Tunaweza Band (Tanzania), Staff Band Namasabo (Tanzania), Lelelele Africa (Kenya), Atemi & the Ma3 Band (Kenya), Sauda (Tanzania).Sherehe za mwaka huu zitafunguliwa na maonyesho mbalimbali ya kuvutia, muziki wenye nakshi mbalimbali ikiwemo nyimbo za kiswahili, madansa, maonyesho ya vipande vya filamu za muziki kutoka Tanzania, Uganda, DRC, Ivory Coast na Senegal.Wakati huohuo, tamasha litadhamini Busara Xtra, yaani matukio ya nje ya tamasha yatakayoandaliwa ndani ya Zanzibar na ambayo yatawavutia na kuwanufaisha wageni waalikwa.Hii itatoa fursa kwa wasanii wa ndani kuonyesha kazi zao, kuwahamasisha wageni kuendelea kutazama maeneo mengine ya visiwa na kuongeza kipato kwa watu wengi.

Post a Comment

1 Comments

Anonymous said…
Thank you for such a well-written and interesting post. I'll surely add it to my Favorites. sildenafil citrate