AIRTEL YAANDAA BONANZA KWA WANAHABARI

Mutta Muganyizi kulia na Beatrice Singano wakizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani.

Kwa mara nyingine tena kampuni ya Simu ya Airtel imeandaa bonaza kwa wandishi wa habari litakalofanyika Februari 12 katika viwanja vya Posta Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana katika mkutano na waandishi wa habari Mkuu wa Habari na Mahusiano wa Airtel Mutta Muganyizi alisema tamasha hilo linatarajiwa kuwakutanisha wanahabari kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari.
Naye Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Airtel Beatrice Singano Mallya alisema hatua hiyo ni ya kuimarisha ushirikiano baina ya Airtel na vyombo vya habari nchini na kwamba bonanaza hilo litaziwezesha pande hizo mbili kufahamiana na kuendeleza mahuziano zaidi.
Alisema wanahabari wamekuwa na mchango mkubwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii na kwamba Airtel wameona kuwa katika moja ya njia ya kuonyesha thamani waliyonayo wanahabari kwa kukutana na kuburudika kwa pamoja kupitia michezo.
“Ni kawaida kwatika kila mwisho au mwanzoni mwa mwaka kufanya thamini ya jumla ya pale tulipo na wapi tunakwenda lakini pia huwa tunakitumia kipindi hiki kuka na kufurahi kwa pamoja na watu wenye majukumu tofauti katika kulijenga taifa ambapo miongoni mwao ni ninyi wanahabari” alisema Singano.
Aliongeza kwa kusema wameandaa burudani kadhalika kutakuwa na michezo mbalimbali ya kubahatisha ambapo wanahabari wataweza kujishindia zawadi tofauti kutoka Airtel.
Michezo itakayokuwepo ni pamoja na mpira wa miguu, pete, kuvuta kamba, mbio za magunia kuimba na kucheza muziki wa dansi.
Alisema taratibu nyingine kuelekea katika tamasha hilo ziendelea kutolewa kadri siku zitakavyosonga ambapo ameahidi wanahabari kupata burudani ya aina yake katika tamasha hilo .
“Airtel imedhamiria kuwapa wanahabari burudani ya pekee kwani mchango wenu umekuwa wa kipekee”alisema Singano.
Hii ni mara ya pili kwa Kampuni ya Airtel kuandaa bonaza kwa wanahabari nchini , Kampuni hii ilibadilisha jina lake (Nembo) yake mwaka jana kutoka Zain na kufahamika kwa jina la sasa.

Post a Comment

0 Comments