Pichani ni Anna Mc Catney kutoka Mradi wa kutokomeza Malaria,United Against Malaria ambao ni moja ya wadhamini katika Michuano ya Kombe Tusker 2010 inayoanza Jumamosi Novemba 27 ameahidi kutoa elimu bora kwa wanamichezo kuhusu kupambana na ikibidi kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria barani Afrika.
Aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari ulioratibiwa na Kampuni ya One Plus chini ya Mkurugenzi wake Fina Mango.
“Tunaamini kwa kupitia wanamichezo ambao wananguvu ya kutosha katika kufikisha ujumbe kwa hadhira juu ya kupambana na kujilinda na Malaria ndiyo sababu kubwa iliyotusukuma kutoa udhamini katika michuano hii ya CECAFA 2010”
Kutokana na michuano ya CECAFA kuwa na nguvu, tutaendelea kutoa elimu kwa timu shiriki za mashindano ya CEFAFA namna ya kujikinga na Malaria.
“Mpango huu wa kupambana na Malaria umekuja Afrika Mashariki na Kati ambapo pia zinaonyesha vifo watu wazima na watoto milioni 38.9 wanaugua na ugonjwa huo huku watu 209,000 wakifa kila mwaka”.
0 Comments