YANGA NA LAMBALA WALAMBA MILIONI 31.5 TANGA

Na Safari Chuwa, Tanga

Pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga ya jijini Dar es Salaam na Azam FC ‘Wanalambalamba’ lililopigwa kwenye Uwanja wa Mkwawani jijini hapa umeingiza zaidi ya sh milioni 31.5.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi mjini jana, Meneja wa Uwanja wa Mkwakwani, Mbwana Msumari, alisema katika pambano hilo lililomalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu na kwenda sare ya bila kufunga, watazamaji 8,244 waliingia kwa kukata tiketi na kuwezesha kupatikana kwa mapato hayo sh 31,514,000.
Kutokana na mapato hayo, kila timu imeweka kibindoni shilingi 6,933,000 huku fedha nyingine zikienda kwenye makato mengine kama gharama za uwanja na mambo mengineyo.Uwanja wa Mkwakwani unaotumiwa na Azam FC kama uwanja wa nyumbani baada ya ule wa Uhuru wa jijini Dar es Salaam kufungwa kutokana na ukarabati, umekuwa na mahudhurio mazuri kiatika mechi za Ligi Kuu hasa zinapocheza timu maarufu za Simba na Yanga

Post a Comment

0 Comments