WASHINDI NANE WENYE VIPAJI KUCHUANA KATKA SWAHILI FASHION

Hatimaye majina ya wabunifu 8 wenye vipaji ambao wameingia fainali na kushindania zawadi ya mwaka katika onyesho kubwa la wiki la mavazi Swahili Fashion Week 2010 wapatikana.

Uchaguzi wa wabunifu wa mavazi wanaochipukia umefanyika Septemba 10 katika hotel ya Southern Sun jijini Dar es salaam, ambapo majina 8 yalichaguliwa na jopo la majaji wanne ambao ni Jamila Swai ambae ni mbunifu wa mavazi hapa nchini, Mkurugenzi wa Sanaa Nsao Shalua kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (National arts Council), Michelangelo Adam kutoka ubalozi wa Italia hapa nchini na Mustafa Hassanali.


Wabunifu hao 8 waliongia fainali watashindana katika kuonyesha kazi zao katika onyesho kubwa la wiki la mavazi Swahili Fashion Week litakayofanyika mwezi wa Novemba mwaka huu.

Mratibu wa Swahili Fashion Week, Ndugu Washington Benbella amesema kuwa “ Wabunifu wote 16 walikuwa wazuri na wameonyesha vipaji vya hali ya juu, na kuonyesha kuwa Tanzania ina vipaji vikubwa katika sanaa ya ubunifu wa mavazi”.

Wabunifu wa mavazi wanaochipukia waliofanikiwa kuingia fainali ni pamoja na Pooja Narendrakumar Jeshang, Abduel Urassa, Shaban Mfaume, Kelvin Boniface, Subira Rahma Wahure, Angelina Muna and Grace Kijo.

Majaji walikuwa na kazi ya ziada, kwani walikuwa makini katika kuangalia mambo mbalimbali ili kuweza kupitisha majina 8 ya wabunifu wa mavazi wanaochipukia, kwani walilazimika kuangalia uwezo katika ubunifu na kuchora, kwa kiasi gani mchoro unavitia, rangi iliyotumika katika mchoro na mambo mbalimbali yanayohusiana na ubunifu kwa ujumla.

Sahili Fashion Week ni jukwaa pekee linalowaleta pamoja wabunifu wa mavazi na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya Kiswahili, ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira, sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maoneo hayo wanayoongea lugha ya Kiswahili, sambamba na kuhimiza dhana nzima ya kuthamini bidhaa zinazotengenezwa Afrika Mshariki.

Msisitizo zaidi umewekwa katika kuhakikisha kwamba sekta ya ubunifu inakuwa kikanda. Swahili Fashion Week inalenga kukuza sanaa ya ubunifu na kuwa jukwaa bora la kibiashara kimataifa kwa nchi za Afrika Mahariki.

Kwa mara ya tatu sasa Swahili Fashion Week imekuwa ikifanyika, ambapo kwa mwaka huu itafanyika November 2010, Dar Es Salaam, Tanzania.

Shindano hili linafanyika kwa mwaka wa tatu sasa, halina kikwazo cha umri, na linatoa fursa kwa watu wote wanaoamini kwamba wana kipaji cha ubunifu, na wanataka kuwa wabunifu. “Swahili Fashion Week ni jukwaa bora kwa wabunifu kuonyesha uwezo wao wa ubunifu na kuibua sindano la wabunifu wapya, ni jukwaa linalowawezesha watu kufikia malengo yao ”, aliongeza Mustafa Hassanali muandaaji wa Swahili Fashion Week.

###
Saphia NgalapiMedia & PR ManagerMustafa HassanaliPO Box 10684, Dar es Salaam, Tanzania105 Kilimani Road, Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania(opp. Patricia Metzger Health & Beauty Clinic / near French Embassy)Tel : +255 (0)22 266 8555Mobile : +255 (0)712 099 834Mail : media@mustafahassanali.net Web : http://www.mustafahassanali.net/http://www.swahilifashionweek.com/http://www.harusitradefair.com/
www.twende.info
.

Post a Comment

0 Comments