Social Icons

Friday, October 1, 2010

Wakali wa Salsa kung'arisha Tamasha la Shear Ball 2010

Msanii Doram Melanie akiwa na mwenyeji wake Penzi wa Shear Magazine hapa wakiwa nje ya ukumbi wa Irish Pub Msaki, Melanie naye ni mkali wa kusakata Salsa nilimwona jana usiku anatishaa kinoma.
Nnaemek Joshua Amaechi ambaye ni mwanamuziki pia mwalimu wa kucheza katika miondoko ya Salsa kutoka nchini Ireland ametua nchini kwa kunogesha Tamasha la kutima mwaka mmoja kwa Jarida Bomba la mitindo na nywele la Shear Magazine, hafla itafanyika katika hoteli ya Doule Tree Masaki Dar es Salaam Oktoba 2. Mgeni rasmi ni Mshauri wa Rais Januari Makamba pia wageni na watu mashuhuri watakuwepo ndani ya hafla. Hivyo Blog hii ikiwa nmji mmoja kati ya wadau wa karibu wa Shear Illusions nakuahidi kumwagia mapicha na kila litakalojiri usiku huo maridhawa.Wageni wote watakuwa katika mavazi ya rangi nyeupe na nyeusi. Zulia Jekundu kama kawaida.Tiketi hazitauzwa mlangoni kiingilio no USD 100.Bendi ya Banana Zorro na wasnii wa Nyumba ya Vipaji (THT) watakuwepo. Tamsha hili limedhaminiwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania na 88.4 Clouds FM.

No comments:

 
 
Blogger Templates