WABONGO WAJIKITA KATIKA UJASIRIAMALI WA MANENO

Dina http://www.mamapipiro.blogspot.com/ hapa anawakilisha kuwa NDIVYO NILIVYO,na hakika kila mtu ndivyo alivyo mumuache.
Lebo yake ni DODO GEAR na anauza mwenyewe ukihitaji mpango mzima unatafuta chaguo lako, hata kwa oda ya jina utakaopenda .Zamani ilikuwa maneno kama haya utayakuta katika Khanga lakini hivi sasa hapa kwetu Dar es Salaam na Tanzania nzima kwa ujumla imekuwa ni mtindo unaokua kwa kwasi.
Makuburi Akionyesha Lebo ya DODO GEAR yaani ni bonge la CHATA.
Hapa unaambiwa'IKIZIMIKA PAPASA' aliyetinga anaitwa Makuburi Ally a.k.a Wakudikulika.
Mamaa KhadijaLinda sipitwi hapa nawakilisha na SISHOBOKI inakwenda sambamba na mimi mwenyewe kwa wanaonijua abadan huwa Sipendi Shobo na ukizileta SISHOBOKI.
Kwa nyuma Nembo ya DODO GEAR, Jamani Bongo Tambarare wanaovaa maneno katika Khanga na sisi kwenye fulana ujumbe unafika na kama utasema ooh mambo ya Kiswahili alokwambia sisi ni wadhungu nani kwani hujui kuwa Uswahili ni jadi yetu PENDA CHAKO ENH na MDHARAU KWAO AU CHAKE NI MTUMWA.
MBALI YA SISHOBOKI pia zipo zenye majina na maneno mbalimbali kama vile WEWE TU MIMI SINAHABARI na nyingine nyingi.
Hellen Goromera a.k.a DADA yeye amechagua jina linalokwenda sambamba na kazi yake zaidi hapa anasema TUNAKESHA KAMA CNN hii inawafaa wanahabari na wote mmeiona enh hizi zinauzwa na mjasiriamali ambaye pia ni mchora vibonzi (katuni) Said Michael ak.a WAKUDATA.
Hapa Hellen akionyesha nembo ya WAKUDATA COMIC WEAR.
WAKUDATA Orijigo, Mchora Vibonzo ( Katuni), licha ya kuuza naye anajipendelea .

Post a Comment

0 Comments