Kampu ya Bia ya Serengeti kwa kupitia bia yake ya Tusker jana imetangaza rasmi kudhamini michuano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Tusker Challenge Cup 2010) , udhamini wenye thamani ya sh milioni 675.Akizungumza leo katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya New Afrika Meneja Mawasiliano na Masoko Teddy Mapunda alisema udhamini huo utasaidia Shirikisho hilo la mpira wa miguu la Afrika Mashariki na Kati kugharamia tiketi za ndege kwa washiriki , maofisa wa CECAFA pamoja na marefa, malazi usafiri wa ndani , uratibu , zawadi , ada mbalimbali, usalama, gharama za kutumia uwanja, usajili wa waandishi wa habari na gharama nyinginezo.Alisema michuano hiyo ambayo imepangwa kuanza kati ya Novemba 27 hadi 11 mwaka huu itazihusisha timu za Burundi, Djibouti,Somalia, Ethiopia, Sudan, Zanzibar,Eritrea,Kenya, Uganda, Rwanda, wenyeji Tanzania na kwa mara ya kwanza CECAFA imealika timu ya taifa ya Ivory Coast kama timu alikwa pia timu ya Cameroon nayo wanatarajiwa kuthibitisha kushiriki kwao wiki ijayo.
DKT. NCHEMBA AMUAGA BALOZI WA MAREKANI NCHINI
-
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema kuwa
Tanzania ina thamini mchango mkubwa wa Taifa la Marekani ka...
4 hours ago
0 Comments