Wachezaji wa Timu ya Taifa 'Taifa Stars' wakisikiliza mawaidha ikiwa ni siku mbili kabla ya kukipiga na Morocco .
Kocha Mkuu wa Taifa Stars Poulsen akijinasibu kwamba vijana wake wako gado kwa mtanange na Morocco utakaopigwa siku ya Jumamosi.
Makabidhiano ya Jezi anayepokea ni Nahodha wa timu Shadrack Nsajigwa, Naibu Katibu Mkuu Sunday Kayuni na Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Mawasiliano NMB Iman Kajula na mwenye njano ni Poulsen akishududia.
Ikiwa ni katika maandalizi ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Benki ya NMB jana imetoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. Milioni 10.Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo na Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini TFF Sunday Kayuni amewataka wachezaji hao kutumia hamasa na maoni waliyopewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Michezo na Utamaduni Joel Bendera siku chache kabla ya kwenda kukipiga na Algeria.“Chukueni mifano ileile ya Naibu Waziri Bendera mkacheze katika mtindo uleule mliocheza Algeria nina imani kubwa mtashinda na kuwaambia wapeni raha watanzania1” alisema Kayuni.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano NMB Imani Kajula alisema udhamini huo ni mwendelezo wa Benki hiyo kwa Taifa Stars huku akisema vifaa walivyotoa ni pamoja na seti za jezi watakazo vaa katika mechi, mipira mitano, jezi za kuvaa wakiwa kalba ya mechi, Traksuti 30 nguo za kuvaa nje ya uwanja wanapokuwa pamoja viatu jozi 30 ambavyo ni vya mazoezi na mechi.Naye Kapteni wa Taifa Stars Shadrack Nsajigwa ambaye alizungumza kwa niaba ya wachezaji wengine alisema anatoa shukrani kwsa NMB kwa udhamini wao na kuwasaidia bila kuchoka.“Tumejiandaa vizuri hivyo napenda kusema kwamba sisi Taifa Stars tumejiandaa vyema na tutajitahidi kadri ya uwezo wetu kufanya vizuri katika mechi hii” alisema Nsajigwa.

0 Comments