KAIJAGE AONDOKA NA MOROCCO


SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limemsimamisha kwa muda wa mwezi mmoja, Ofisa Habari wake Florian Kaijage baada ya tukio la kutoimbwa kwa nyimbo za Taifa katika mchezo kati ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars na Morocco katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki kombe la Mataifa ya Afrika.

Siku ya Jumamosi , tarehe 9 Oktoba 2010, tumeshuhudia fedheha ya kushindwa kutimiza itifaki muhimu ya kupiga nyimbo za taifa husika, yaani nyimbo ya taifa ya Morocco na nyimbo ya taifa ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Hilo lilikuwa ni tukio la aibu sana kwa nchi yetulililofanyika mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania , Mhe Jakaya Mrisho Kikwete , mbele ya halaiki ya wapenzi wa mpira wakiwemo wageni wetu wakiongozwa na Balozi wao.Lakini pia , kwa vile mchezo huo ulionyeshwa katika luninga ndani na nje ya nchi , tukio hili la aibu limeshuhudiwa pia na Watanzania nchini kote na wapenzi wa mpira duniani.

Jambo la kusikitisha ni kuwa tukio hilo halikustahili kutokea.Kwa kuwa tatizo la nyimbo za taifa kutopigwa ipasavyo katika michezo ya kimataifa lilishawahi kutokea .Jitihada mahsusi zilizfanywa kuhakikisha kuwa safari hii jambo hili halitokei.Wahusika walipewa jukumu la kuhakikisha kuwa wanazijaribu nyimbo hizo siku mbili kabla ya mchezo na kuhakikisha kuwa hakuna hitilafu yeyote itakayotokea.Wahusika walifuatiliwa kwa karibu na kila walipoulizwa walikuwa wakijibu kuwa wamesha hakikisha kuwa hakutatokea dosari yeyote.

Kushindwa kupiga nyimbo za taifa kama ilivyopangwa ni upungufu mkubwa kiutendaji na kama nilivyosema hapo awali, aibu kwa taifa letu.Kufuatia tukio hilo , awali ya yote napenda kwa niaba ya TFF , kuomba radhi kwa mheshimiwa Rais wetu , wapenzi waliofurika uwanjani, Watanzania kwa ujumla na wageni wetu kutoka Morocco.

Aidha napenda kuwahakikishia wapenzi na Watanzania kwa ujumla kuwa tukio kama hili halitatokea tena. Kuanzia sasa, hata kama mitambo ya uwanjani ni mizima patakuwepo pia bendi ya polisi/jeshi (brass band) ama mitambo ya tahadhari (stand by facilities) kwa ajili ya nyimbo za taifa na matangazo mengine muhimu.

Mwisho, tukio hili ni kubwa. Haliwezi kwisha hivihivi bila ya wahusika kuwajibika .tumewasiliana na viongozi wa Wizara yetu ya Michezo kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina unafanyika kubaini nini hasa kilichotokea.

Pamoja na hatua hiyo TFF imechukua hatua ya awali ya kumsimamisha kazi mhusika wake mkuu katika suala hilo, Ofisa wa habari Florian Kaijage kuanzia leo hii. Tumemwajibisha kwa vile yeye ndiye aliyekuwa amepewe jukumu la kusimamia jambo hilo. Wakati amesimamishwa Kaijage ataisadia timu itakayoundwa kufanya uchunguzi kamili wa tukio hilo. Hatua zitachukuliwa kwa yoyote atakayebainika kuhusika na kutokea kwa tukio hilo.

Post a Comment

0 Comments