MAREHEMU ABDALLAH RAMADHAN
Kituo cha Luninga cha Channel TEN na Redio ya Magic FM cha jijini Dar es salaam kimepata msiba kwa kuondokewa na mmoja wa watangazaji wake mahiri na vijana, Abdallah Ramadhani (Pichani) ambaye amefariki dunia katika ajali ya gari Ijumaa iliyopita .
Marehemu Abdallah Ramadhani aliyezaliwa 1980 alipata ajali hiyo akiwa njiani mjini Beira, Msumbiji akitoka nchini Afika Kusini kurudi Tanzania Alhamisi tarehe 7 mwezi huu.
Taarifa zaidi zinasema kuwa marehemu alikuwa kwenye gari aina ya Toyota Prado ambayo ilipasuka tairi la mbele na kupinduka mara kadhaa na hivyo kusababisha kifo chake mara baada ya kufikishwa hospitalini.
Mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo iliyompasua kichwa, familia yake ilifahamishwa ambapo mdogo wake aitwae Hussein alikwenda kumuangalia hospitali alikolazwa kabla ya kufariki.
Abdallah atakumbukwa na watazamaji wa Channel TEN kwa usomaji wake wa taarifa za habari kwa umakini na ufasaha na kwa wasikilizaji wa Magic FM. Kabla ya kufikwa na mauti, alikuwa katika mapumziko ambayo aliyatumia kwenda nchini Uingereza kwa siku kadhaa kabla ya kupitia Afrika Kusini ambako alipumzika kwa siku chache na baadaye kuamua kurudi nchini kwa njia ya barabara kupitia Msumbiji.Marehemu anazikwa leo Dar es Salaam pia ameacha mke na mtoto.
Pole kwa ndugu, jamaa na wanahabari wote kwa ujumla na wale wote walioguswa na msiba huu.
Apumzike pema Abdallah Ramadhani.
INNA LILLAH WAINNA ILAIHI RAJIUN
DKT. NCHEMBA AMUAGA BALOZI WA MAREKANI NCHINI
-
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema kuwa
Tanzania ina thamini mchango mkubwa wa Taifa la Marekani ka...
6 hours ago
0 Comments