Pia sehemu ya fedha hizi zilizotolewa zilitumika katika kugharamia safari ya walimbwende wote 30 waliotembelea hifadhi ya wanyama kama Serengeti, Manyara, Bonde la Ngorongoro na kwenye Mapango ya Amboni Tanga.
Aidha, kabla ya kumpata Balozi huyu pia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kupitia Bodi ya Utalii iliandaa semina kwa walimbwende hao kuhusu utalii wa ndani pamoja na shindano la kumtafuta Balozi wa Utalii wa Ndani 2010, semina hiyo ilifanyika Septemba 6 mwaka huu katika Hoteli ya Giraffe View iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Katika semina hii mada mbalimbali zilitolewa juu ya maana ya utalii, utalii wa ndani, taasisi zinazosimamia sekta ya utalii nchini , aina za utalii , watalii faida za utalii wa ndani na vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini ambapo mwakilishi wa TTB aliweza kuzungumzia pamoja na mambo mengine ikiwa ni pamoja na majukumu ya TTB.
Kadhalika warembo hao walifundishwa juu ya mbinu za utangazaji wa utalii wa ndani pamoja na changamoto zilizopo katika kukuza utalii wa ndani nchini.
Aidha, wakati mada zikitolewa washiriki waliweza kuuliza na kujibu maswali yaliyodhihirisha upeo wa juu wa masuala ya utalii wa ndani.
Mambo yaliyojitokeza kwenye majadiliano haya ni pamoja na umuhimu wa kuimarisha miundombinu, juhudi za TANAPA na NCCA kuhifadhi na kukuza utalii, changamoto za kifedha kwa wananchi, umuhimu wa kutangaza utalii kwa wananchi wengi na kwingineko ikibidi hata katika shule zote ambazo ni zile za awali, msingi, sekondari na vyuo vikuu .
Nzuki anasema kuwa baada ya semina, waliendesha mchakato wa kumtafuta balozi wa utalii wa ndani kwa kuwataka warembo kujibu maswali kutoka kwa jopo la majaji na ndipo Mwakalukwa akachaguliwa na kutangazwa siku ya fainali za shindano hilo.
“Tulimchagua mrembo huyu kutokana na jinsi alivyoweza kujibu kwa ufasaha pamoja na vigezo vingine tulivyokuwa tumeviweka hivyo atakuwa na taji hili kwa kipindi cha 2010 hadi 20111” alisema Nzuki.
Anamalizia kwa kusema kuwa hivi sasa Bodi ya Utalii inakamilisha taratibu za mkataba wa maelewano na Balozi huyo ili aanze kazi za kutangaza utalii wa ndani kutokana na jinsi atakavyopangiwa.
Akipokea hundi yake yenye thamani ya shilingi milioni 2,900,000 Hapa Mwakalukwa akikabidhiwa Laptop aina ya Dell (Window 7) yenye thamani ya shilingi Mil 1,1000 na Dk. Nziku wanaoshuhudia tukio hilo adhimu kutoka kushoto Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency Hashim Lundenga, Salma, na Ofisa Masoko wa Bodi ya Utalii David Meena.Pia Dk Nziku amesema kwamba wataendelea kudhamini shindano la urembo la Miss Tanzania kwa miaka mingine 2 ijayo ambapo kwa mwaka huu udhamini wao ulikuwa wa kiasi cha shilingi milioni 122,000. Pia walikuwa na Kauli mbiu isemayo UTALII WA NDANI UANZE KWA MTANZANIA MWENYEWE.
0 Comments