Hapa Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki Ole Loibanguti , Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Hashim Omaruy, Meneja wa NMB Tawi la Mkuranga Wirra Said Wirra waliosimama huku wanafunzi kutoka kushoto Akwino Leonald anayesoma darasa la 3, Hassan Rajab darasa la 6 na Aisha Said wakiwa wameketi katika dawati mbele ya chumba cha darasa moja lililojengwa na NMB na kupiga picha ya kumbukumbu shuleni hapo.
Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki Ole Loibanguti akiwa amekaa katika dawati moja kati ya 30 yaliyotolewa na NMB .
Shyrose Akisalimia wakina mama na wazazi wa wanafunzi waliofika kushuhudia tukio hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Henry Clemence akipeana mkono na Mkuu wa Kitengo Cha Mahusiano NMB Shyrose Bhanji ambaye pia alikabidhi moja ya madawati 30 yaliyotolewa na Benki ya NMB yaliyotolewa msaana katika shule ya Shule ya Msingi Mlaleni iliyopo Mkuranga Mkoa wa Pwani.Mbali ya Madwati pia NMB wamejenga darasa moja vyote vikiwa na thamani y a shilingi milioni 3 aliyesimama katikati ni Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki Ole Loibanguti akifuatiwa na Meneja wa NMB Tawi la Mkuranga Wirra Said Wirra na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Hasim Omary.
Kikundi cha ngoma kilitumbuiza kikundi cha burudani kinachoundwa na wasanii wanne cha Ngoma ya asili cha ‘Ngoma Sita’ kilikonga nyoyo wakati kilipotumbuiza katika mtindo wa ngoma aina ya mdundiko kabla na baada ya makabidhiano hayo.kutoka shoto wasanii wanaounda kundi hilo ni Amanzi Ally, Suleiman Abdallah na Mohammed Omari.
Shyrose akizungumza mbele ya hadhira ya wanafunzi, waalimu na wakazi wa kata ya Mlaleni.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo Henry Clement, amewapongeza NMB, huku akiwasisitiza wakazi wa eneo hilo kujivunia msaada huo walioupata.Clement, alitoa wito kwa wananchi waliohudhuria hafla hiyo na Wanafunzi kukataa kuwa wasindikizaji wa elimu na kuwataka watumie vyema madarasa pamoja na madawati katika kupata elimu bora watakaoleta maendeleo katika siku za usoni.
Hemed Said Mwanafunzi wa Darasa la 6 akipionyesha umahiri wa kupiga danadana.
Gender Balance hapa mtoto Akwino naye akapokea mpira akiwakilisha watoto wanafunzi wa kike yeye hakupiga danadana bali alirusha juu kisha akaudaka kana anacheza netball.
Ukafika wakati wa kula kuku hapa ilikuwa ni kuku wa Kienyeji siyo Droiler's wa Bongo na hapa mimi na Ofisa Uhusiano Doris Kilale a.k.a WIFI tulikuwa katika hoteli moja ambayo inamilikiwa na Mheshimiwa mmoja ni maarufu sana Mkuranga ambayo pia inakuja kwa kasi tembea uone jamani manake ilibidi nivue miwani ili nidadavue vizuri kuku.
Ofisa Habari wa NMB Shyrose Bhanji na Mimi.
Wadau hili gari lilikuwa limepaki pembeni mwa barabara ambapo wakati tunapita tulilikuta yakikuwa matatau na wakati tunarudi tena looh kuuliza tukaambiwa uzito umezidi hivyo jamaa wa Mizani Mkuranga wakawa wamewazuia mpaka tulipoondoka hakukuwa na dalilizozozte za kuondoka kwa wakati huo japo jamaa walitujia juu kwa nini tunawapiga picha bila kibali wakasahau kwamba walikuwa katika kingo za barabara.Binafsi naihurumia nchi hii kila siku tunakata miti hebu tujiulize ni miti mingapi inapandwa kabla ya kukata na magogo kusafirishwa nje ya nchi.
0 Comments