Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia mradi wake wa maji ujulikanao kama 'HAKUNA MAJI,HAKUNA UHAI' umesaini mkataba wa shilingi milioni 31.9 na kikundi cha wajasiriamali cha MSABI kilichopo Ifakara mkoani Morogoro.
Pichani Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TBLrRobin Goetzsche pichani akikabidhi mfano wa hundi kwa wawakilishi wa kikundi cha MSABI katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya TBL jana Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Robin Goetzche akishikana mkono na mwakilishi wa MSABI.Kikundi hicho cha MSABI kinaunganisha vijana wa rika mbalimbali kutoka Ifakara na kwa kupitia mkataba huu kikundi hicho kwa ushirikiano na TBL itashirikiana katika kuchimba visima 10 ambapo shule 10 zilizoko kwenye vijiji 5 vitafaidika.Kazi zitakazofanywa na kikundi ni pamoja na kuongeza ujuzi wa watu wa vijiji husika katika kutengeneza , kutunza visima hivi vitakavyokuwa vinaendeshwa kwa kutumia kamba ya mikono kwa kusukuma maji.Kwa kuhakikisha maji yanayovunwa kwenye visima vitakavyochimbwa ni safi na salama, mtambo wa kupima ubora wa maji utanunuliwa kwenye mradi huu.Pamoja na hayo shule nyingine mbili zitafaidika kwa kujengewa vyoo kwa makadirio ya kutumiwa na watu zaidi ya 700.

Post a Comment

0 Comments