BENDI ya muziki wa dansi ya Kalunde imepata mwaliko wa kwenda kutumbuiza jijini Maputo nchini Msumbiji.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Rais wa bendi hiyo, Deo Mwanambilimbi alisema kuwa, watatumbuiza nchini humo Oktoba 2 mwaka huu.Mwanambilimbi alisema, wanatarajia kuondoka nchini Oktoba Mosi wakiwa na wanamuziki wao wote.“Tumepata mwaliko wa kwenda kutumbuiza kwenye moja ya tamasha, ambalo hufanyika kila mwaka, hivyo tunatarajia kwenda kupiga nyimbo zote za Kalunde,” alisema Mwanambilimbi.Alisema, mwaliko huo umekuja kutokana na baadhi ya mashabiki wa bendi hiyo, kuvutiwa na nyimbo wanazopiga.Kalunde kwa sasa inatamba na vibao kama ‘Itumbangwewe’, ‘Hilda’, ‘Nataka Kuzaa na Wewe’ , ‘Usiniguse’ ,’Fikiria’, ‘Kilio Kilio’ na vipya ‘Fungua’ na ‘Maiwane’ ambazo tayari zimeanza kutamba katika kumbi mbalimbali za burudani ambazo bendi hiyo inatumbuiza.Baadhi ya wanamuziki watakaoondoka na bendi hiyo ni Mwanambilimbi mwenyewe, Shehe Mwakichui, Junior Gringo, Deborah Nyangi, Sarafina Mshindo, Mwapwani Yahya, Othman Majuto na Remmy.
UOKOAJI KARIAKOO NI USHUHUDA WA MOYO WA UTANZANIA: NCHIMBI _Apongeza
wananchi wa kawaida kwa kujitokeza haraka kuokoa watu_ _Serikali, vyombo
vyake na taasisi binafsi zapewa heko kwa mwitikio wa mfano_
-
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi
akipokea taarifa kuhusu shughuli ya uokoaji watu inayoendelea katika eneo
yali...
47 minutes ago
0 Comments