Wasanii hili nalo neno!

Wasanii waliouziwa viwanja Mkuranga watapeliwa .
Na Futuna Seleman, Nkuranga
Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA) ambalo linaundwa na wanahabari, wasanii kutoka katika Asasi mbalimbali nchini linadaiwa kutapeliwa mashamba waliyodai kuyanunua katika kijiji cha Mwanzega, Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.Uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Mkuranga,umetoa maelezo kuwa,wale wote waliouziwa mashamba hayo wametapeliwa,kwani Wilaya na Halmashauri hazipaswi kuhusika kwa namna yoyote ile katika mchakato huo.Mkuu wa Wilaya hiyo Henry Clemence amesema tayari Jeshi la Polisi Wilayani humo limeingilia kati na kuwashikilia kwa muda Mwenyekiti wa Kijiji hicho pamoja na viongozi wa asasi hiyo (jina tunalo).
Alisema kuwa hadi sasa Mtendaji wa kijiji hicho hajulikani alipo baada ya kutoroka kwa kujua kuwa anasakwa na vyombo vya dola.Clemence alitoa maelezo hayo wakati akizungumza na Nipashe baada ya watu waliochukuliwa fedha kupitia SHIWATA kutua Wilayani humo kwa lengo la kukabidhiwa maeleo yao . “Wilaya ya Mkuranga haina ardhi kama hiyo Wilaya hii ipo karibu na jiji la Dare Es Salaam inapaswa kupangwa vizuri ili ilete manufaa kwa watu wa Mkuranga.Kwa wanaotaka kuja huku Mkuranganawashauri wafuate taratibu na wasivunje amani iliyopo wanaotaka ardhi wapitie Halmashauri,wasipitie katika asasi wala kwa mtu yeyote kwa sababu taratibu za kumiliki aradhi hazielekezi hivyo,”alisema mkuu huyo.
Habari zaidi inapitakana katika gazeti la Nipashe toleo namba0856-5414 inapatikana katika ukurasa wa 22 .

Post a Comment

0 Comments