FM Academia kuzindua albam Eid Mosi


Kiongozi wa bendi ya FM Academia Nyoshi El Saadat amevunja ukimya na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa albamu ya 6 ya bendi hiyo itakayokwenda kwa jina la 'Vuta Nikuvute' ulipangwa kufanyika siku ya Idd Mosi kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.Albamu hiyo itakuwa na nyimbo 8 ambazo ni majina na watunzi wake wkenye mabano Vuta Nikuvute (Elombee Kichinja), Heshima kwa Wanawake (Rogger Mzungu), Mwili Wangu (Christian Mene Professor), Angalia Shida Yangu (Toscan Nzimbu), Fadhila kwa Mama (Jesus Katumbi), Usiku wa Jumatano (Flora), Mgeni (Jesus Ebonga Katumbi), Jasmin (Nyoshi), Intro Ngwasuma Mthematics Mayemba (Nyoshi), Heineken Ngwasuma (FM Academia), na Moses Katumbi.Aidha albamu ya hiyo mpya itakuwa na Volume (1) na Volume (2).Msanii Nameless kutoka nchini Kenya atakuwa msanii mwalikwa siku hiyo.Pia Nyoshi amesisitiza kuwa albamu ya Vuta nikuvute iko katika kiwango chenye ubora.

Nyoshi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments