Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Leodgar Tenga (Katikati) akitoa nasaha zake kwa wachezaji wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' hawapo pichani wakati akiwaaga ambapo kesho wataondoka nchini kwenda Algeria kuanza Kampeni ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika (CAN).Mechi hiyo itapigwa Septemba 5. Wakati huohuo mdhamini mwenza wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Benki ya NMB wametoa vifaa vya michezo kwa timu hiyo vyenye thamani ya sh.Mil 56.Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika jijini Dar es Salaam Meneja Mawasiliano wa Benki ya NMB Josephine Kulwa alisema kwamba huo ni mwendelezo wa NMB kama wadhamini kutoa vifaa kwa Taifa Stars kila inapokuwa ikikabiliwa na mechi za kirafiki na Kimataifa.Nahodha wa timu hiyo Shadrack Nsajigwa alipokea vifaa hivyo kutoka kwa Ofisa wa NMB kwa niaba ya wachezaji wengine huku akitoa ahadi ya kurudi na ushindi.
MTOTO ALIYEPOTEA MKOANI RUVUMA 2024 APATIKANA, RPC ATOA ONYO KALI
-
Na Regina Ndumbaro Ruvuma
Mtoto Groly, mwenye umri wa mwaka mmoja, ambaye aliripotiwa kupotea mwaka
2024 katika Kata ya Mjimwema iliyopo Manispaa ya Wilay...
24 minutes ago
0 Comments