Wakati Shirikisho la Ngumi za Ridhaa hapa nchini (BFT),likiunda Kamati maalum ya kuchunguza sakata la mgomo wa mabondia wa TANZANIA katika michuano ya ngumi ya Afrika ya Mashariki,baadhi ya mabondia wa timu hiyo wamesema hawakukusudia kugoma bali mazingira magumu ndiyo yaliwafanya washindwe kushiriki katika michuano hiyo.Mabondia hao akiwemo Nahodha wa timu hiyo Joseph Martin na Alphonce Mchumia Tumbo wamesema wasingeweza kushiriki katika michuano hiyo bila kupatiwa mahitaji muhimu ya mchezo huo kama chakula pamoja na posho za usafiri ambalo lilikuwa ni jukumu la BFT.Wachezaji wa timu hiyo hawakutokea katika michuano hiyo ambayo ilishirikisha timu za Uganda, Kenya, Rwanda na Mauritius, huku Tanzania ikiwa mwenyeji.Mabondia hao wameanza mazoezi kama kawaidi huku wakiwa wanasuburi nini viongozi wa BFT wanatarajia kuwaambia mara baada ya kutokea kwa mgomo huo.
0 Comments