Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alli Hassan Mwinyi akifafanua jambo.
Rais mstaafu wa awamu ya pili akizungumza na vyombo vya habari ndani ya ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alli Hassan Mwinyi anayeonekana nyuma yake ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa.Hapa Mwinyi akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mkutano huo kufungwa.
Mwandishi mwandamizi kutoka Daily News akiuliza swali katika mkutano huo leo jioni.
Mwandishi mwandamizi kutoka Daily News Bilham Kimathi akiulizwa swali wakati wanahabari walipopewa fursa hiyo. Mwanablog wa Bongoweekend.blogspot Khadija, Shehe Semtawa kulia na wanahabari wengine kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutanohuo.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Benjamin Mkapa, amezitaka nchi za Afrika kutoogopa kuwapokea na kushirikiana na wawekezaji kutoka China na badala yake ikijikite katika kutazama faida itakazopata.Mkapa alitoa rai hiyo jana katika mkutano wa kimataifa juu ya maboresho ya sera za ardhi barani Afrika, ulioanza juzi na kumalizika jana katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.Akigusia changamoto zinazokabili matumizi ya ardhi, rais huyo mstaafu, pamoja na mambo mengine, alizitaka nchi za Afrika kutoogopa kile kinachoitwa uvamizi wa Wachina wanaowekeza kwa wingi katika bara hili, kwani hiyo inaweza kuwa ni propaganda tu inayojengwa na nchi zinazoihofia China katika ushindani wa kiuchumi duniani.“Msiogope kile kinachoitwa uvamizi wa Wachina, wanaosema hivyo wanahofia umoja wa ushirikiano wa kiuchumi ambao unaweza kuwa na nguvu ya kuwashinda wao… hata kama ni wavamizi, cha msingi ni kutambua maslahi ya taifa tunapoingia makubaliano na wawekezaji lakini tusifikie hatua ya kusema kabisa Wachina wanakuja kutunyonya”, alisema Mkapa.Alisema umiliki na matumizi mazuri ya ardhi barani Afrika yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya kutokuwa na mitaji pamoja na uwezo wa kitaalam na kusisitiza kuwa matatizo hayo yanahitaji kushughulikiwa kupitia maboresho makubwa ya kisera na mikakati ya pamoja.
Kutoka kushoto ni Mchungaji Charles Stith, katikati aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza Mwanamke wa Msumbiji Luisa Diogo na aliyekuwa Rais wa vya Mauritius.

0 Comments