Social Icons

Wednesday, June 24, 2015

BANZA STONE AZUSHIWA KIFO,ASHA BARAKA AKANUSHA

UZUSHI wa kifo cha mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi nchini Ramadhani Masanja Banzastone wawapa mashabiki wa muziki wake taharuki usiku wa jana huku mwajiri wake wa zamani Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka akikanusha vikali kwamba habari hizo zilizozagaa jana usiku ni za uongo.

Akizungumza leo asubuhi kwa njia ya simu Asha alisema kwamba "Huo ni uzushi wa kwenye mitandao Banzastone yu hai licha ya kwamba ana umwa" alisema Asha.


Hivi karibuni iliripotiwa na vyombo vya habari kwamba hali ya mwanamuziki huyo kuwa siyo nzuri kiasi kwamba amegoma kula huku mama yake mzazi akilalamika kwamba wasanii wenzake hawaonekani kumsaidia hivyo anaomba msaada wa hali na mali.

Wakati huohuo mtandao wa Saluti5 unaripoti kuwa Habari hizi si za kweli na ni uzushi wa kipuuzi. Saluti5 imepokea zaidi ya simu 15 zikitaka uthibitisho juu ya habari hizo ambazo sasa zimekuwa kama mazoea juu ya msanii huyo. 

Hii ni zaidi ya mara 10 Banza anazushiwa kifo. Banza Stone yu hai na anaendelea vizuri, Saluti5 imeongea na amesema anashukuru mungu hajambo.

No comments:

 
 
Blogger Templates