Social Icons

Thursday, April 28, 2011

BENKI YA EXIM YAAHIDI KUINUA UCHUMI WA NCHI




Na Mwandishi Wetu


Benki ya Exim imeahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika mikakatimbalimabli ya kuinua uchumi wa nchi.
Hayo yalisemwa jijini jana na Meneja Mkuu wa benki hiyo,Dinesh Arora.

Alikuwa akizungumzia ufadhili wa benki hiyo kwenye mkutano wa uwekezaji Afrika uliofanyika jijini katikati ya mwezi huu na kuhudhuriwa na Maraisi watano kutoka nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki na wajumbe zaidi ya 900 kutoka sehemumbalimbali duniani.Alisema kuwa sekta binafsi inao wajibu mkubwa wa kuisaidia serikali kuinuauchuni na hivyo kuboresha maisha ya Watanzania.



“Exim Benki iliona fahari kubwa kufadhili mkutano huu ambao ulikuwa una lengo la kuonyesha utajiri wa rasilimali za nchi na pia kufungua fursa za kibiashara”,alisema.

Arora alisema kuwa Benki ya Exim itaendelea kusaidia fursa kama hizo ilikuwawezesha Watanzania wengi zaidi kuweza kupata nafasi ya kukutana nawafanyabiashara kutoka sehemu nyingine za dunia.Alisema kuwa benki yake ina wajibu mkubwa wa kuendelea kuisaidia uchumi wa nchi kukua.

Alisema kuwa ili wajasiriamali wa Kitanzaniia waweze kukua kibiashara na kutoamchango mkubwa zaidi kwenye uchumi,lazima ziwepo juhudi za makusudi zakuwakutanisha na wawekezaji kutoka Afrika na duniani kote.


“Tunaamini kuwa maendeleo ya benki yetu yanategemea sana mafanikio ya jamii yetu tunakofanyia kazi”alisema. Alisema pamoja na biashara benki hiyo ina jukumu la kuchangia shughuli mbalimbali za kijamii na kwamba ujasiriamali ni miongoni mwa sekta zinazochangiwa kwa nguvu na benki husika.

“Tumekuwa tunafanya biashara ya kibenki kama jukumu letu kuu lakini pia tumekuwa na majukumu mengine kwa jamii inayotuzunguka hivyo udhamini wetu katika TEYA ni miongoni mwa utekelezaji wa majukumu hayo na kwamba Ujasiriamali tunauangalia kwa namna ya kipekee,” alisema.

Aliongeza kuwa katika kutambua umuhimu wa sekta hiyo,hivi karibuni wamefungua akaunti mpya ya Tumaini maalumu kwa ajili ya Wajasiriamali wanawake.

Alifafanua kuwa pamoja na wengine wanawake ni mhimili mkuu wa shughuli za kijamii katika familia nyingi za kitanzania hivyo benki hiyo imeona ipo haja ya kipekee kuwawezesha ili nao waweze kumudu majukumu yao kwa ufanisi.

Kuhusu tuzo hiyo alisema ni changamoto ya kutosha kwa Wajasiriamali nchinikatika kuhakikisha shughuli wanazozifanya zinakuwa na tija kwao binafsi na taifakwa ujumla.

“Akaunti ya Tumaini ni maalumu kwa ajili ya Wajasiriamali Wanawake na hii inaonyesha jinsi tunavyoijali sekta hii lakini pia tuzo hii ni changamoto kubwa kwa wahusika kwani itawasukuma kufanya shughuli zenye tija,” alisema Arora.

TEYA imelenga kutambua kazi za Wajasiriamali katika nyanja mbalimbali kutokanana mchango wao katika pato la taifa na ukuaji wa uchumi lakini pia kutoa changamoto ya ushindani kwa wahusika na sekta ya kibiashara kwa ujumla.

TEYA 2011 ilizinduliwa rasmi Machi 15 mwaka huu na inatarajiwa kutolewa baadaye Novemba ambapo Raisi Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Mawazo Waziri

Media Relations Manager Capital Plus International (CPI)

Phone:022 2125431 , Cell: +255 715 027 892,

+255 754 027 892

+255 684 000 645

No comments:

 
 
Blogger Templates