Social Icons

Thursday, April 28, 2011

MAWAKALA MISS TAZANIA KUPIGWA MSASA KESHO

LINO INTERNATIONAL AGENCY LIMITED
P.O. BOX. 53069 DAR ES SALAAM, TELEFAX :+255 22 2120201,
SAMORA AVENUE AND MKWEPU, MOBILE: +255 753 764156, DAR ES SALAAM.
Email: mailto:linotz2000@yahoo.com misstanzania@email.com
http://www.misstanzania.net/


REF: ILA/ PR.10/VOL.2/68 27 April 2011


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

YAH: SEMINA YA MAWAKALA WA MASHINDANO YA UREMBO YA MISS TANZANIA 2011.
Tafadhali husika na kichwa cha habari hapo huu,
Semina ya Mawakala wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2011 itafanyika tarehe 29 na 30 April 2011 katika hotel ya Paradise City iliyopo Posta jijini D’salaam.
Semina hii itahusisha Mawakala wote wa Mikoa, na Kanda wanaoandaa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.
Katika semina hiyo ambayo pia itakuwa ni Mkutano wa mwaka wa Waandaaji wa Miss Tanzania katika ngazi za Mikoa na Kanda, mambo kadhaa yatazungumzwa ikiwemo, kukumbushana Kanuni, Sheria na Taratibu za Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, maadili na miiko ya uongozi, na uendeshaji wa mashindano.
Pia Changamoto mbalimbali zinazokabili mashindano ya urembo zitajadiliwa.
Mada mbalimbali zitatolewa na Wataalamu kutoka katika Fani ya urembo na Taasisi mbalimbali. Pichani kulia ni Miss Tanzania anayemaliza muda wake Genevieve Mpangala
HASHIM LUNDENGA.
MKURUGENZI.

No comments:

 
 
Blogger Templates