Hayo yalisemwa na katibu wa kikundi cha Eddy Charity cha Kibaha, Edgar Mwakalosi wakati kilipotembelea kituo cha Kisarawe Safe House na kutia misaada mnalimbali
Naye Meneja wa kituo hicho Florida Frank alisema kuwa mbali ya changamoto mbalimbali kubwa ni kwa madarasa ya mtihani ambapo huwabidi kukaa kambini hasa wale wa kidato cha pili na cha nne kwani kwa sasa wanapaswa kulipa shilingi 60,000 kwa mwanafunzi mmoja na wako wanne.
Alisema kuwa jamii inapaswa kupandikiza kitu muhimu katika maisha ikiwa ni pamoja na kuwezesha kwenye suala la elimu kituo hicho kikianzishwa mwaka 2003 kikiwa na watoto watano na sasa kina watoto 48 wanaosoma elimu tofauti hadi vyuo vikuu.





0 Comments