Wazanzibar husema, Zanzibar ni njema atakaye aje, Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ni miongoni mwa Taasisi zilizoshiriki tamasha la Kizimkazi 2026 na kukakabidhiwa cheti kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutambua ushiriki wa mamlaka hiyo ambayo imevutia maelefu ya wananchi kushuhudia vivutio vya utalii mubashara katika viwanja vya maonyessho.
Kupitia Luninga (Screen) kubwa iliyofungwa katika viwanja vya maonyesho hayo ilikonga nyoyo za waliotembelea tamasha hilo kwa kuona wanyama wakubwa watano ambao ni Tembo, Chui, Nyati, Simba, Faru pamoja na makundi ya wanyama wengineo waliopamba Ngorongoro wakionekana katika mazingira yao ya asili.

0 Comments